Karibu kwenye rasilimali za Mafunzo ya Redio kwa Wakulima

Njia za kujifunza na kujua ni nini wasikilizaji wa kipindi chako wanahitaji

September 1, 2021

Ili uweze kutengeneza kipindi cha redio cha kilimo chenye kukidhi mahitaji ya wasikilizaji unapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:
1) Jitahidi kufahamu wasikilizaji wako; 2) Famahu taarifa/habari za kilimo zenye umuhimu kwao; 3) Famamu namna ya kuwashirikisha wakulima ipasavyo kwenye majadiliano ya redio juu ya mambo muhumi wanayoyaona.

Mifumo ya muingiliano kuwatia moyo wasikilizaji kushiriki

August 31, 2021

Programu za muingiliano ni zile zinazohusisha au kuvutia mawasiliano ya pande mbili kati ya kituo cha redio na wasikilizaji wake. Mawasiliano hayo yanaweza kuwa ya ana kwa ana, kupitia simu, ujumbe wa maandishi au barua au inaweza kuwa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na njia zingine za mawasiliano mitandaoni. Mawasiliano hayo ya pande mbili yanaweza kuwa kati ya msikilizaji na mtangazaji, msikilizaji na mwanasiasa, msikilizaji na wakala wa uenezaji, msikilizaji na mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali au kati ya wasikilizaji wawili au zaidi.

Kufanya kazi kwa kuzingatia umbali kama mtangazaji wa redio

June 1, 2020

Wakati mwingine, watangazaji wa redio hawawezi kuripoti habari kwenye eneo la tukio au kwa kukutana uso kwa uso na watu wanaohusika. Hii ni kweli hasa wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) wakati serikali ulimwenguni kote zimetunga sera ambazo zinahitaji watu kuweka umbali wa mita moja kutoka kwa kila mtu isipokuwa wale wa nyumbani kwao ili kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi.

Tafuta

Kategoria za aina na

Chuja

Zaidi ya vituo 1,000 vya redio barani Afrika hupata fursa za kujifunza na kutumia rasilimali zetu za mafunzo . Na wanakuwa wadau watangazaji.