Jinsi ya kuandaa kipindi bora cha simu za wasikilizaji

Simu za redioni ni nini?

Simu za redioni ni mfumo unawawezesha wasikilizaji wa kipindi kuweza kuchangia maoni juu ya mada wakati wa kipindi. Simu za redioni za wasikilizaji zinaweza kuwasehemu ya kipindi, au inaweza kuwa ni sehemu ya kipindi. “Simu za redioni mara nyingi watu wanaita Simu za wasikilizaji.” Maneno haya mawili yanamaanisha kitu kimoja.

 

Itanisaidiaje kuwahudumia wasikilizaji wangu wakulima?

 • Inaongeza taarifa katika kipindi change kwa kujumuisha maoni ya wakulima.
 • Inawasaidia wasikilizaji wangu kuunda maoni juu ya mada muhimu.
 • Inawajumuisha wasikilizaji wangu na kuwapa nafasi ya kuzungumza katika kipindi juu ya mada muhimu, na kuweza kusikika.
 • Inawasaidia wanajamii kupiga hatua katika kutatua tatizo.
 • Inawapa nafasi wanajamii kutoa hisia zao juu ya jambo lililo wagusa.

 

Inawezaje kunisaidia mimi kuandaa kipindi bora?

 • Inatoa uhakika juu ya umuhimu wa mada, na kuniwezesha kuamua kuendelea kuongelea mada au kusitisha kuongelea mada.
 • Inanitambulisha kwa wasikilizaji wenye maarifa, wenye maoni,wenye maelezo ya ufasaha ambao ninaweza kuwahoji katika vipindi vinavyokuja. (Chukua namba zao za simu na mahali wanapoishi.)

 

Ninaanzaje? (Jifunze kuhusu haya na maelezo Zaidi hapa chini.)

 1. Chagua mada inayowavutia wasikilizaji wako na yenye kuwaunganisha wasikilizaji wako.
 2. Uliza maswali.
 3. Mualike mtaalamu mwenye mchango.
 4. Weka maoni yawe mafupi.
 5. Ifuate sharia nan chi husika.

Malezo ya kina

1. Chagua mada inayowavutia wasikilizaji wako

Baadhi ya simu zinagusia mada za muhimu (mfano., “Kwanini mavuno ya mahindi yalikuwa machache msimu huu?”)

Simu zinasaidia jamii kufikisha hisia zao (kwa mfano, inawaruhusu wakulima kupiga simu na kutoa heshima zao kwa kiongozi aliye tangulia mbele ya haki).

Baadthi ya simu nyingine ni kwaajili ya burudani tu (mfano., “Nani ni mchezaj bora nchini?”)

Mada inapaswa kuwa ni mada ya kusisimua na inawagusa wasikilizaji.

2. Ongeza uzito kwa kuweka swali.

Kama mada ni juu ya upungufu wa mavuno ya mahindi, basi waulize wasikilizaji waulize maswali yenye kugusa hisia zao kama: “Je uliuza mahindi ya kutosha kuweza kulisha familia yako?”Waulize wasikilizaji wote hili swali na waruhusu wazungumze kwa kina wakueleze tatizo lilikuwa ni nini. Msikilizaji anapopiga simu redioni useseme tu, “Hello” na moja kwa moja kumuacha azungumze. Muelezee mpigaji simu juu ya mada na mpate swali na mpe muda alijibu.

3. Mshirikishe mtaalamu mwenye maarifa juu ya mada husika.

Simu za wasikilizaji ni moja kati ya chanzo cha mwanga na hamasa juu ya mada. Mwanga unaweza ukaanza kwa mgeni aliyealikwa katika kipindi mwenye uelewa mkubwa wa mada na ambaye anaweza kutoa maelezo na taarifa bnafsi zinavyohitajika. Mara nyingi tarifa za ziada zinaweza kutolewa na wasikilizaji walio guswa na mada.

4. Weka maoni yawe mafupi na yakueleweka.

Simu za redioni ni nafasi inayowapa wasikilizaji fursa ya kurusha maoni yao . Mara nyingi sio vizuri kumuacha msikilizaji mmoja kushikilia kine na kuongea kwa muda mrefu kiasi cha kuwazuia wasikilizaji wengine wenye maoni kushindwa kuchangia mada. Baathi ya wasikilizaji wengine wanapenda kuongelea mada zao wanazo penda— na wasijibu swali husika. Unapaswa kuwarudisha kuongelea mada husika. Kwa mfano unaweza kusema: “Bi. X, muda mwingine tunaweza kuzungumzia kuhusu mbuzi wanao shambulia busatni,lakini leo, unaweza kuwajulisha wasikilizaji kuwa ulivuna kiasi gani cha mahindi?”

Fuata mashari na sharia ya nchi yako.

Baathi ya nchi, simu za redioni haziruhusiwi kabisa, na kituo cha habari kinaweza kupoteza leseni yake ya kurusha matangazo. Kwa baathi ya nchi simu za redioni zinasikilizwa kwanza na kutoa maneno kabla ya kurusha hewani. Kwan chi nyingine majina na namba za msikilizaji aliyepiga simu zinatajwa hewani, jadili na meneja wa kituo kujua sharia zilizoko katika eneo ulipo.

Mambo mengine ya kuzingatia yanayoweza kufanya kipindi cha simu redioni kuwa kipindi cha kuvutia

Jiandae!

Hivi ni vipindi vya moja kwa moja. Unavyo kuwa unafikiria nini kinaweza kujitokeza wakati wa kipindi ndivyo unakuwa umejiandaa vyema kuweza kukabiliana na matokeo yanayojitokeza wakati wa kipindi. Hii ni muhimu sana hasa hasa kipindi chako cha simu za redioni kinaongelea mada nyeti/tata kama vile “Je mumbe wa halmashauri anawasaidia wakulima?” Maandalizi ya mada kama hizi zinajumuisha:

 • Kuwaanda watu ambao unaweza kuwategemea kuwa na maoni tofauti juu ya mada hii ili kuweza kusaidia kuendesha majadiliano.
 • Fikiria maoni makali wasikilizaji watakayo yatoa na angalia namna unayoweza kuyajibu na kuendesha kipindi.
 • Jiandae kupata maoni tofautitofauti, kama wasikilizaji wakiwa wanazungumzia kitu kimoja tu.

Elewa majukumu na changamoto za mtangazaji.

Kuendesha kipindi hiki cha simu za redioni kunachangamoto nyingi, na inahitaji mbinu nyingi kuweza kufanya: ni lazima:

 • kujua mada vyema
 • wasaidie wasikilizaji kuelezea mada zisizo eleweka vizuri
 • kuweza kutambua matatizo mapema kabla haijaenda mbali
 • kuwa rafiki, mpole na pia kuwa na msimamo
 • onyesha hisia kwa kiwango na kwa wakati, (kwa mfano, kufurahi kwenye simu na msikilizaji kwa wakati muafaka na kuwa na msimamo pale inapokulazimu)
 • usichague upande na jaribu kupata maoni ya pande zote mbili
 • nukuu suala muhimu lililo tajwa na msikilizaji na omba msikilizaji aweze kuelezea
 • uwe na uwezo wa kutumia muda endapo hakuta kuwa na simu zinazoingai
 • tambua muda alioutumia msikilizaji kwenye line na tafuta namna ya upole ya kumuaga
 • … na zaidi!

Waheshimu wapiga simu.

Kumbuka kuwa huna kipindi pasipo wapiga simu! Wasikilizaji watapiga simu kama wakisikia kuwa wasikilizaji wengine walio piga simu walihudumiwa vyema. Washukuru wasikilizaji kwa kupiga simu. Na kama hawaja zoea kuzungumza hewani basi wape moyo, na wasaidie waweze kutoa maoni yao vyema. Kama mtu akipiga kwa mara ya kwanza, onyesha furaha, itawashawishi wasikilizaji wengine kupiga simu.

Kukabiliana na taarifa zisizo rasmi na hazina uhakika.

Kama msikilizaji ameeelezea jambo muhimu kama ambalo halina utambuzi wa uhakika, usi waache wasikilizaji wadhanie kuwa jambao hilo ni kweli moja kwa moja, tafutia ufumbuzi na usiache tu wasikilizaji wakachukulia kuwa ni ukweli kwasababu tu imeruka redioni.

Kwa mfano, Kama msikilizaji akisema, “Wpte tunajua kuwa hela zote za hamashauri zimetumika kanda ya kusini,” na kama huwezi kuhakiki au kusahihisha kauli hii, unaweza kusema kitu kama: “Bw. Inoussa, hiyo ni kauli nzito umeisema, sijui kama ni kweli au si kweli. Labda wasikilizaji wengine wanaweza kukubaliana na wewe au kupingana na wewe.” Kama mnakitengo cha waandishi watafiti katika kituo chenu cha redio unaweza kusema hivi,: “Bw. Inoussa, kauli yako ni nzito sana, sina uhakika lakini nitawapatia watafiti wetu taarifa hii na watafanya utafiti na tuta tangaza jambo hili katika kipindi kijacho.”

Mtumie msaidizi.

Unaweza ukawa na kazi nyingi, unapokea simu na kuendesha kipindi. Ni vigumu kufanya mambo yote tajwa hapo juu na kuongea na wasikilizaji, mtafute msaidizi akusaidie kujibu simu za wasikilizaji. Msaidizi wako anaweza kusoma meseji zinazoingia na kuchagua meseji nzuri za kusoma katika kipindi.

Chuja simu zinazoingia.

Kama una line Zaidi ya moja na simu zinaingia nyingi, ni vyema kuchagua simu gani utazirusha hewani. Pia inasaidia kupunguza simu za wasikilizaji wanaongea mada isiyo husika, anaye chagua simu za wasikilizaji anaweza kupata taarifa za ziada kama, majina kamili, mahali wanapoishi na namba zao za simu na mambo muhimu wanayoyazungumza, usikate simu ya msikilizaji kwasababu tu haukubaliani na maoni yake.

Kuepusha usawa wa kijinsia kwa kuwa na simu mbili.

Kwa kawaida wasikilizaji wanawake wako mbali na simu kuliko wasikilizaji wanaume.na pia wana kosa muda wa kuweza kupiga simu, mara nyingi wakijitahidi kupiga mara moja au mara mbili wanakata tamaa kuendelea.Kuwa na simu mbili, simu moja utawapa nafasi wanawake tu kupiga kwa kufanya hivi utaweza kuwapa asilimia 50 nafasi wanawake kutoa maoni redioni.

Tumia nafasi hii ya kipindi cha simu redioni kuelimisha jamii.

Mara nyingine unaweza kutumia nafasi hii kuwasaidia jamiii kupata utatuzi wa jambo na kuwasaidia kusonga mbele juu ya mada muhimu. Mfano kama swali lako ni, “Afisa ugani alikutembelea kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita?”na kama wasikilizaji wengi wakisema hapana, hii inawapa nafasi serikali kuu kuwasukuma maafisa ugani kuwatembelea wakulima.Na kama swali lako ni, binti yako amekuwa akisumbukiwa njiani wakati anaenda shuleni?” na kama wasikilizaji wengi wanasema ndio, basi jamii itajua ina tatizo la kutatua.

Tangazi kipindi chako.

Tangaza kipindi chako kwa kupiga promo kabla ya kipindi na wape wasikilizaji swali kabla ya muda wa kipindi wapate muda wa kutafakari.

Kuwa mwangalifu na simu zinazotoa sifa kwa mtu flani.

Mara nyingine mtu mwenye madaraka atampatia mkulima simu na kumwambia amsifie katika kipindi, bila hata kujali mada inayoongelewa.Si sahihi kumpata muda wa mazunguzo msikilizaji kama huyo. Kwa upole muulize msikilizaji kama anaweza kujibu swali lililo ulizwa na kama hataki kuzungumzia swali basi moja kwa moja nenda kwa msikilizaji mwingine.

Kuwa mwangalifu na wapigaji wa simu mara kwa mara.

Kama lengo lako ni kupata sauti nyingi redioni iwezekanavyo basi hutotaka wasikilizaji wachache kumiliki line ya simu. Lakini pia kama unawajua wasikilizaji wano piga simu mara kwa mara na kutoa maoni mazuri na kupendezesha kipindi, basi tafuta namna ya kuwa ruhusu waongee—endapo tu wanafuata sharia zako na kujua muda wanao paswa kuzungumza.

Punguza gharama za wapiga simi.

Tafuat huduma za bure ambazo wasikilizaji wanaweza kupiga simu bila kuchajiwa. Hii itawavutia wasikilizaji wengi na kuwapa uhuru wa kutoa maoni yao.

Usitoe mawazo potofu!

Kama wasikilizaji 8 wamepiga simu redioni na kusema kuwa wamepata mavuno madogo ya mahindi msimu huu, usichukulie kwamba watu nane kati ya kumi katika eneo hilo wamepata hasara au mavuno machache ya mahindi msimu huo.” Unachoweza kusema baada ya kipindi ni kuwa watu nane kati ya watu kumi walio piga wamepata mavuno macheche msimu huu. Ambacho huwezi kusema ni kwamba 80% wamepoteza mavuno yao msimu huu.”

Kipindi cha simu redioni sio utafiti unaofanyika nyumba kwa nyumba huwezi kutoa takwimu kamili Msikilizaji:

 • lazima awe na simu ya mkononi
 • lazima ajiandae kulipia simu (endapo tu simu ni bure)
 • awe huru na kujiamini kuongea na uma
 • aweze kusikiliza kipindi

Kwa maneno mengine, aliye piga simu sio mwakilishi wa jamii nzima.

Pia, kwa mada za kisiasa, watu huwa wanapenda kupiga kulingana na namna walivyoshawishika. Mara nyingine kipindi kinakuwa kimewagusa watu wanaotaka mabadiliko, watu wengi ”walio kimya “—wasikilizaji walio ridhika na hali iliyopo wanapelekea kuwanyamazisha hata wale wenye kutaka mabadiliko—hivyo hawata piga simu.

Waambie wasikilizaji sharia.

Kipindi cha simu redioni kina hitaji sharia chache ili kiwe bora. Wafahamishe wasikilizaji wako sharia hizo ni zipi awali. Sheria zinaweza kuwa rahisi kama hivi:

“Tunapenda kupata maoni ya wasikilizaji wengi iwezekanavyo, na tunawaomba wasikilizaji leo wakioiga simu wazungumzie mada husika tu. Tuta pokea simu za wasikilizaji ambao hawakupiga simu kwa kioindi cha miezi mitatu iliyopita. Na kumbuka kuwa Zoom FM haiito vumilia lugha chafu, matusi au vichocheo vya ugomvi.”

Kutokana na kwamba wasikilizaji wanajua sharia zao (kwasababu unazirusha kila wiki), haita kuwa mbaya kama unapopokea simu na kumkumbusha msikilizaji kwa kusema, “Bi. Muta, unafahamu sharia zetu. Lazima nikate simu yako sasa na nipokee simu nyingine. Nina waomba radhi wasikilizaji kwa kauli hizo za Bi. Muta.”

Anza kidogo.

Kama hukuwahi kuendesha kipindi cha simu redioni, anaza na mada nyepesi zisizo na utata kama, “Mavuno yako ya mahindi ni mazuri msimu huu kuliko mwaka jana?” Kwa uzoefu unaopata, unaweza kuanza kufanya mada ngumu,kama “usambazaji wa mbolea na serikali unakusaidia?” au “kiongozi mteule anakusaidia?”

“Kuwa msatari wa mbele.”

Kama unataka wasikilizaji wako kutoa maoni mazito katika kipindi chako basi wewe kuwa wa kwanza kutoa maoni yako mazito. Tembelea vijijini na rekodi mahojiano “vox pop”. Waulize watu maswali yatakayo kuwa yanaulizwa redioni kwa kipindi kijacho. Chagua mada ya kuvutia na kauli nzito itakayo sukumu na kuhamasisha kipindi kwa wiki nzima na kasha tegemea maoni ya upinzani kuendesha kipindi chako.

Epuka ukimya.

Hakuna kitu kibaya kama kukosa wasikilizaji watakao piga simu! Hii inaweza kuwa kwasabu mada haina mvuto au inaweza kuwa wasikilizaji wanataka kusikia mada kabla ya kupiga simu redioni. Hii hapa namna ambayo unaweza kuepuka hli.

 • Chagua mada na swali vizuri.
 • Mualike mtaalamu mwenye maarifa juu ya mada na anweza kutoa mchango wakati unasubiria simu kupigwa.
 • Kuwa na “vox pop” zilizo rekodiwa tayari kwa kuzi cheza.
 • Waandae watu wawili au watatu ambao wanaweza kucnngia.
 • Muanda mtu studio ambaye unaweza kuzungumza nae.

Jifunze kutoka kwa wasikilizaji wako pia.

Kipindi cha simu redioni ni sehemu pia ambayo unaweza kujifunza kuwa wasikilizaji wako wanataka nini. Lakini isiishie hapo tu, tembelea vijijini kutana na wakulima wanawake na wakulima wanaume, waulize maoni yao. Angali hapa kujifunza juu ya utafiti wa wasikilizaji.

Kuwa makini na mazungumzo yanayo changia fujo.

Mazungumzo yanayo plekea fujo moja kwa moja yanaweza kuwa (mfano, “Wa Zumu wameiba ardhi yote yenye rutuba.”) Lakini watu wanao taka kufikisha ujumbe wa chuki siku zote wanazungumza kwa kuwalenga kikundi fukani: Unapogundua kauli kama hizi unaweza kujibu kama “Bw. Kalo, Najua wewe pia usingependa kama mtu angezungumza hivyo juu yako pia. Tuendelee na msikilizaj mwingine, ambaye ni …” Ulizia kama watangazaji wengine walisha wahi kupata malalamiko kutoka kwa msikilizaji huyu, na andaa sera yenu redioni ambayo itawawezesha kuepuka mijadala inayochochea ugomvi.

Je, wasikilizaji wanaopiga simu redioni lazima wajitambulishe?

Wasikilizaji wengi wanao piga wanapenda kutoa majina yao na mahalai wanapoishi. Lakini mara nyingine wasikilizaji wanapenda kuficha majina yao na mahala wanapoishi kuepuka matatizo hasa hasa pale wanapotoa maoni juu ya mada tata kwa upande wa pili hutakiwi kuwa nyamazisha watu ambao wamejihisi kutishiwa.

Uhitaji kutangaza majina yao na mahali wanapoishi, ila unapaswa kunukuu majina yao na mahali wanapoishi( hapa utaona umuhimu wa kuwa na msaidizi katika kipindi) . Msikilizaji kama huyu unaweza kumtambulisha kama ifuatavyo,: “Sasa tunaweza kumsikia mwanamke aliye kuwa na uzoefu mkuwa wa eneo hili, na ameomba majina yake yasitaje.”Ukifuata utaratibu huu, itakusaidia kupata wasikilizaji wa aina nyingi wenye maoni ya aina mabali mbalimbali.

Kwa baathi ya mada ambazo ni tata, unaweza kuwajulisha wasikilizaji mapema kuwa kama zinavyodai sheria ni vyema tukajitambulisha majina yetu kabla hatujatoa maoni yetu, unaweza kuanza kipindi kwa kusema “Kutokana na kwamba mada hii ya leo ina utata mkubwa, na tunapenda kufuata sheria zote, leo tutawaomba wasikilizaji wote kutoa majina yao kabla hawaja toa maoni yao redioni.”

Wapi ninaweza kujifunza Zaidi kuhusu kipindi cha simu a wasikilizaji?

- Internews yametoa namna tofauti ambayo unaweza kuendesha kipindi shirikishi. Unaweza kusoma katika tovuti hii: http://www.internews.org/research-publications/interactive-radio-toolkit-stations

Maana ya maneno

Mfumo ni namna halisi ambayo maneno na sauti yanandaliwa kwaajili ya kuumika redioni.Mfumo inajumuisha, mahojiano, maswali na majibu, maigizo, vox pops, simulizi, machapisho, rekodi ya mazungumzo, majibizano na mtangazaji, nk.

Maswali na majinu ni mfumo ambao kituo cha redio kina mualika msikilizaji kuweza kujibu swali husika kwa kupiga simu. Kituo cha redio huwa kinatangaza matokeo ya kura katika kipindi

Promo ni ujumbe mfupi ulioandaliwa kwa makusudi ya kuongeza wasikikilizaji kwa kuwahimiza wasikilize kipindi chako redioni

Sheria na vigezo ni taratibu za nchi zilizowekwa kwa waandishi wa habari kuzifuata kulingana na lesini ilivyotolewa. Nchi inaweza kukipa kituo cha redio onyo, kutoza malipo ya faini, na kuifungia kwa muda au kufunga kituo cha redio moja kwa moja kama hakitakuwa kikifuata sheria.

Kipengele ni sehemu ya kipindi.

Ukaguzi kabla ya kurusha hewani Kipindi cha namna hii ni kipindi kinachotumia teknolojia inayochelewesha maneno kwa sekunde 10 baada ya kuzungumzwa kabla ya kurusha ili kuruhusu kituo kukagua kama kuna maneno mabaya yaliyoruka katika kipindi kabla ya kuruhusu hewan, mfano msikilizaji anaweza kupiga simu na kutoa maoni mabaya kama matusi au yasiyo yakisheria.

Vox pop ni aina ya kipindi ambapo mtangazaji anaenda vijijini na kuwauliza wasikilizaji amaswali mbalimbali kuhusu mada husika. Rekodi ya majadiliano mara nyingi ina haririwa kufupisha na kuhakikisha inaongelea mada husika, na majadiliano haya yanatangazwa wakati wa kipindi husika kinaporuka. (Vox pop ni neno la kilatini linalo maanisha “sauti ya watu.”)

 

Shukrani

Imechangiwa na: Doug Ward, Mwenyekiti wa Bodi, Farm Radio International, na kuongezewa taarifa na Charles Shanks, Mwandaaji mwandamizi, “Uangalizi kwa nchi nzima, maonyesho ya wazi ya Kikanada” Redio CBC, na kutoka kwa Liz Hughes, meneja mstaafu wa waandishi wa habari kituo cha CBC na mwanachama wa bodi ya Farm Radio International.

   Mradi umefadhiliwa na msaada wa kifedha na serikali ya Kanada kupitia kitengo cha mahusiano ya kimataifa (GAC)

This resource was translated into Swahili with the support of USAID’s New Alliance ICT Extension Challenge Fund, through the International Fund for Agricultural Development in Tanzania. For more information about the Fund, please see: https://www.ifad.org/