F.A.I.R. viwango bora vya uandishi wa vipindi vya kilimo kwa waandishi wa habari

Utangulizi

Mwana 2008, Shirika la Farm Radio International lilitambulisha viwango vya V.O.I.C.E. Kwa waandishi wa habari wa vipindi vya wakulima. Viwango vya V.O.I.C.E. Inawasaidia waandishi wa habari kuandaa vipindi vyenye taarifa kamili,inawapa wakulima nafasi ya kuweza kutoa taarifa zao, na kuwavutia wasikilizaji wengi. FRI pia inatoa fomu ambayo waandishi wanaweza kufanya tathmini ya vipindi vyao, kwa kuzigatia viwango vya V.O.I.C.E.

Watangazaji wa vipindi vya kilimo pia wanapaswa kufikia viwango. Watangazaji wanaweza kuwahudumia wasikilizaji vyema endapo vipindi vyao vinatoa taarifa fasaha juu ya mada husika—kama muda wa kupanda au muda wa kutumia mbolea , au jinsi ya kuchanganya mbolea, au nani wa kumpigia wakati wa dharura. Watangazaji wanaweza kumhudumia mkulima msikilizaji vyema kwa kuchambua mambo kwa kina pia. Wasikilizaji wataipendelea redio inayowahudumia na wanayoiamini—kituo kinachotoa taarifa fasaha na maoni mbalimbali—kwa uaminifu.

FRI inataka kuwasaidia waandishi wa habari kupata Imani ya wasikilizaji wao. Hii ndio maana tunawapatia viwango vya F.A.I.R. Viwango vya uandishi wa habari za kilimo. Tunatumaini kuwa watangazaji na waandishi wataweza kujifunza chochote katika mfumo huu. Tuna himiza watagazaji na waandishi kutupatia maoni yao juu ya mfumo huu wa F.A.I.R. Ili tuweze kuboresha.Tafadhli tuma maoni yako kupitia radio@farmradio.org.

Viwango vya F.A.I.R. kwa waandishi wa habari za kilimo

Hivi ni viwango ambavyo mwandishii wa wa habari wa kilimo anapaswa kutumia katika kazi yake:

Haki na Usawa: Simulizi na vipindi vyangu ni vya haki na usawa. Nina maoni mbambimbali na ninaheshimu haki ya wasikilizaji wangu kupata nafasi ya kusikia pane zote mbili za simulizi.

Usahili: Taarifa ninayo tangaza ni ya kweli, taarifa zake ni taarifa zilizofanyiwa uchunguzi. Nina wakilisha ukweli na ninaweak wazi kipi ni taarifa za fasaha na yapi ni maoni.

Ukweli: Ninasimamia ukweli na uhakika pasipo kuchagua pande wowote juu ya mada yeyote, hasa hasa mada inapokuwa na utata. Ninapo chagua upande ni kwa lengo tu la kuendeleza mjadala. Kama nina jambo binafi juu ya mada inayozungumziwa, nitaweka wazi kwa wasikilizaji. Na kama kituo change cha redio kina manufaa binafsi juu ya mada tata inayozungumzwa nitaweka hili wazi pia.

Heshimu: Nina waheshimu wasikilizaji wanao zalisha chakula kwa familia zao na kwa jamii nzima, mara nyingi katika kipindi kigumu. Nina heshimu utofauti wa wasikilizaji wangu na sioonyeshi ubaguzi wowote wa kijinsia, utaifa, rika,dini,makabila,tamaduni,Imani au vikwanzo vyovyote nina wachukulia wasikilizaji wangu wote kuwa ni watu sawa na kipindi changu kina onyesha kuheshimu maoni na mawazo ya wasikilizaji wote.

Haki na usawa

Simulizi yangu na vipindi vina zingatia usawa. Ninawakilisha maoni mbalimbali na ninaheshimu maoni ya wasikilizaji kutoka pande zote

Haki na usawa ni chimbuko la la tarifa yoyote. Wasikilizaji wangu wanategemea hili na wanapaswa kujua taarifa fasaha na vyanzo fasaha, hasa hasa kwa mada tata na mada muhimu. Kwa uhalisia, kipindi kizuri cha kilimo kina wakilisha pande zote mbili wa mada tata kwa haki na usawa ambapo itawasaidia wasikilizaji kufanya maamuzi yao.

Ingawa siku zote sio rahisi kupata usawa katika kipindi kimoja kulingana na vikwazo vilivyopo, kutokuwepo kwa wageni, au mambo mengineyo. Hali kama hii, Nitaweza kupata usawa wa mambo katika vipindi mablimbali—kipindi kimoja kinaweza kuonyesha undani wa jambo moja na kipindi kinachofuata kikaonyesha suala lingine.

Kuonyesha haki na usawa haimaanishi kupokea mawazo na maoni na kukubali pasipo kuhoji, mara nyingi vipindi vya kilimo wakulima wanamtegemea mtangazaji kuweza kuuliza maswali magumu ili kuonyesha undani wa jambo, onyesha kuchambua Imani inayokubalika na jamii kwa muda mrefu au kauli ya mtaalamu

Usawa pia unamaanisha ninawawakilisha wasikilizaji ambao wana mambo ya ziada kuchangia katika mada, ambao hawana ujasiri wa kuzungumza katika redio au kutoa maoni yao.

Ninahitaji kutunza majina ya mtu ambaye anafikiri akitambulika kwa kutoa maoni Fulani kuhusu jamii anaweza akadhurika. Ingawa nitahakikisha maoni ya mtu huyu yanasikika na nitawaelezea wasikilizaji kuwa mwenye maoni ameomba jina lake lisitumike. Kwa hali kama hii nitazungumza na mtangazaji mwenye kuheshimu kanuni za utangazaji na mwenye kuweza kutunza siri, kabla ya kufanya maamuzi.

Nitakuwa mwangalifu kurusha maoni mazito, hasa hasa yale ambayo yanaweza kuwakera watu Fulani au kikundi Fulani cha watu, au kuchochea fujo. Hakuna nafasi ya ugomvi au fujo katika kipindi ha haki na usawa. Kwa kusikitisha, redio inaweza kuwa chombo chenye nguvu kubwa katika kuanzisha malumbano na chuki na mtu anaweza kuingiwa na taama au shauku ya kufanya hivi. Utangazaji huu ni ukiukaji mkubwa wa viwango vya FAIR. Endapo mgeni katika kipindi akisema kitu kibaya cha kuchochea fujo sita kiruhusu kipite redioni. Nitamuuliza mgeni maswali ya kina, kama mgeni hatakuwa tayari kutoa maelezo ya kina na kukanusha jauli yake basi nitasitisha mahojiano moja kwa moja.

Ninapokuwa naangalia kwa umakini namna ninavyotoa muda kwa wageni wenye maoni mazito vile vile nina chukua muda na kuwa makini kuangalia kwa makini chanzo cha maoni chochezi.

Kuna mazingira ambayo haki na usawa vinahitaji uangalizi mkubwa kuliko kawaida, kama kipindi cha uchaguzi. Kwa mfano panaweza pakawa ni suala la muhimu katika uchaguzi na wanachama tofauti wa wanaweza kuwa na pande tofauti na mtazamo tofauti.Lazima niwakilishe mitazamo hii tofauti kwa haki na usawa pasipo kuangalia upande mmoja. Kama kituo change cha redio kina milikiwa na mgombea mmoja wapo basi nitawajibika kuwafahamisha wasikilizaji wangu.

Haki na usawa inahitaji fikira za ndani, kwa mfano, panaweza pakawa na wagombeaji wawili au watatu wenye uwezo wa kushinda uchaguzi. Panaweza kuwa na wagombea wengine watano au sita wasio na uwezekano wa kushinda uchaguzi. Lazima nitumie uwezo wangu kuamua ni kiasi gani cha muda nitawapatia wagombea wenye nafasi kubwa ya kushinda na wale wagombea wenye nafasi ndogo ya kushinda. Kwa manufaa ya wasikilizaji wangu nitawapatia muda wale wenye nafasi kubwa ya kushinda pamoja na wale wasio na nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi.

Pia nitaonyesha haki na usawa katika simu zinatopigwa na mahojiano ya vox pop. Ni vyema siku zote kusikia mawazo ya watu tofauti yakitolewa. Lakini ni vyema kukumbuka kuwa simu za redioni na mahojiano ya vox pop sio taarifa za kisayansi zilizofanyiwa utafiti. Kama, wakati wa simu za redioni, wapiga simu wote watano wanatoa maoni yanayofanana, hii haimaanishi kuwa wote wana maoni hayo. Inamaanisha tu wati watano ambao wamepiga simu muda huo wanamawazo yaliyofanana. Simu hizi zinaweza kuwa zimepigwa na wasikilizaji wenye uwezo mkubwa za kifedha kuliko wasikilizaji wengine, wenye elimu kubwa nap engine ni wa jinsia ya kiume tu. (Hawa ni watu ambao mara kwa mara wanashiriki katika kupiga simu redioni).Nitafanya jitihada za bnafsi kuhakikisha ninawafikia wasikilizaji wasio na uwezo wa kupiga simu redioni, kwa mfano kuwatembelea vijijini. (Hii imejadiliwa kwa kina Zaidi katika chanzo hiki cha FRI chanzo cha taarifa jinsi -ya kupokea simu redioni.)

Usahihi

Taarifa ninayo itoa ni sahihi, iliyofanyiwa utafiti. Nina fikisha taarifa zote zilizopo, ninaweka wazi yapi ni maoni, mtazamo na ipi ni ukweli.

Ninafanya utafiti kuhaikisha kuwa ninatoa taarifa sahihi nay a ukweli kwa wasikilizaji wangu. Kwa mfanoo katika kipindi cha utabiri wa hali yahewa na taarifa za masoko nina hakikisha kuwa taarifa ninayotoa ni sahihi na inatoka katika chanzo kinachoaminika. (Kama taarifa ninazotoa ni za uongo na zimepitwa na muda nina jua zita poteza uaminifu wa wasikilizaji wa kipindi change na kituo cha habari.)

Ninapo kusanya taarifa kutoka kwa watu wengine, Nina tumia fikra zangu—na kufanya utafiti kama inavyo hitajika—kuona kwamba mtazamo wa mtu ni wa kweli au si wa kweli.

Inapobidi, nitasema chanzo change cha taarifa na nitaeleza upande ambao mwenye taarifa anaupendelea.

Kwa mfano, ninapo toa simulizi la mkulima’ maandamano yanayo himiza maboresho ya barabara, Sito sema kulikuwa waandamanaji 200 endapo nilikuwepo hapo na nikawahesabu, au palikuwepo na mtu pale ninaye muamini ambaye alihesabu au alifanya makadirio ya karibu. Kinyume na hapo nitasema, “Kulingana na walioona palikuwa na waandamanaji 200.” Au, vizuri zaidi, “Waandamanaji walifikia 200,” kama aliye panga maandamano ndiye aliye toa taarifa.

Hata hivyo hakuna kitu kizuri kama kuweza kusema: “Nilikuwa hapo na hiki ndicho nilichokiona.”

Taarifa fasaha ni rafiki yangyu. Inazipatia simulizi langu uhalisia na matokeao. Kwa mfano, kama ninafanya taarifa inayoonyesha jinsi mabadiliko ya hali ya nchi yanavyo upandaji wa mazao katika msimu, Ninaweza kusema kwa urahisi, “Kipindi cha upandaji kimeatjiriwa na mabadiliko ya hali ya nchi kwa miaka kumi iliyopita.” Lakini itavutia Zaidi kama nikiweza kusema: “Takwimu za hali ya hewa kwa miaka Zaidi ya 10 zinaonyesha kupungua kwa asilimia 40 za mvua na kipindi kifupi cha miaezi miwili cha upandaji.”

Nita onyesha taarifa za kina kupinga Imani potofu zilizo zoelekwa, kwa mfano. Kwa mfano, kumekuwa na Imani potofu juu ya kinga ya UKIMWI na Virusi vya Ukimwi, na baathi ya watu wamekuwa wakiamini. Mfano mwingine ni ule wakulima wengi wanaamini kuwa kuchoma mabaki ya mimea shambani kunaogeza rutuba shambani. Na kuna ushahidi kuwa hili ni jambo lakweli. Lakini taarifa za kisayansi zinaonyesha kuwa kuchoma mabaki ya mazao shambani kuna sababisha kupotea kwa rutuba ya udongo.Mfano mwingine: Kuna aina mpya ya mbegu za mihogo iliyoboreshwa ambayo inawawezesha wakulima wa mihogo kuweza kukingana na shambulizi la magonjwa nchini Uganda. Kume kuwa na taarifa kuwa aina hii mpya inasababisha Kansa. Taarifa hizi sio sahihi, lakini ilisambaa kwa wengi. Kufikia viwango bora vya uandishi na utangazaji wa taarifa kituo cha redio kinapaswa kuwa na taarifa za kisayansi na zilizo fanyiwa utafiti kuweza kubadilisha mawazo potofu ya watu.

Katika hali kama hii, Nitaangalia ukweli, kuwatafuta wataalamu, na kuweza kubadilsha madai haya yasiyo ya kweli. Hii ndio maana baada ya kufanya utafiti wa mada hii, Nina weza kusema hivi, “Taarifa zilizopo za kitafiti zinaonyesha kuwa kuchoma mabaki ya mazao shambani mara nyingi kunapelekea kuharibika kwa udongo na kupelekea kupungua kwa uzalishaji kwa kipindi kirefu.” Lakini nitafanya hivi kwa namna ambayo nitakuwa nikiwatunzia wasikilizaji wangu heshima yao. Wanastahili taarifa za ubora na za kweli lakini pia hawapaswi kujisikia kama ninawa dharau

Pia wanaweza kutoa maoni yao, au maoni ya kibiashara au serikali. Inapofaa, Nitawauliza wataalamu kutoa ushahidi juu ya jambo fulani.

Ubaguzi pia ni tatizo linalofanana. Kwa mfano, baathi ya watu wanaamini kuwa wafugaji wote wa kuhamahama ni watu wa asili ya Fulani na kabila hili linapelekea kuzuka kwa matatizo kwa wakulima. Kabila hili na mifugo yao wanapandikizwa kesi nyingi kama wizi, uvamizi wa silaha za moto na ubakaji, kitendo hiki si cha usawa na kinaumiza. Ninapotangaza nitasimamia ukweli na kuepuka kuchochea tabia kama hizi.

Ninawasaidi wasikilizaji wangu kuelewa utofauti baina ya ukweli na maoni, maoni yanathaminiwa sana katika kipindi change cha kilimo redioni maoni yanaonyesha ni kwa jinsi gani mtu au kikundi Fulani kina mtazamo gani juu ya mada fulani,na ni jinsi gani wanaweza kufanya maamuzi juu ya jambo husika, ingawa ni majukumu yangu kuhakikisha wasikilizaji wangu wanaelewa ukweli na uhalisia wa mambo juu ya mada husika.

Nina pelekea ukweli usikike. Kama wasikilizaji’ nitawawakilisha, Nitauliza swali ambalo wasikilizaji wangu wakulima wangeuliza. Mfano, kama kampuni ya mbegu ikisema kuwa mbegu zao zina ongeza uvunaji nitauliza, ushahidi au takwimu ya taarifa hizi. Kama mtaalamu akisema mbinu mpya ya upandaji inaongeza uzalishaji basi nitauliza ushahidi wa mbinu hiyo ikiongeza uzalishaji.

Uadilifu

Nina simama kama mtu mwadilifu na mwaminifu na hata siku moja siwezi kusimama upande mmoja wa mada, hasa hasa katika mada ambazo ni za utata.Ni tasimamia tu kuhimiza majadiliano, Nitajitahidi suala hili lisikike hewani. Na kama kituo change cha redio kina mahusiani na mada inayozungumziwa nitaweka hili sawa.

Nitajitahidi kuto simama upande wowote, na kuonyesha hai na usawa katika vipindi vyangu vyote. Nitafanya kazi kwa makini kwa kujenga jamii yangu, kutafuta ukweli, na kuwakilisha ukweli kwa uadilifu, kwa uhuru na kusimamia maamuzi yangu.

Nitakuwa mwangalifu sana kama nitakuwa na jambo binafsi juu ya mada inayozungumziwa, hii itanisaidia kutokuwa na ubaguzi,Kama kuna jambo nina jua kuhusu mada hii au historia yangu ya maisha inayohusiana na mada husika moja kwa moja nitaweka wazi.Kwa mfano kama nilikuwa nikifanya kazi na kampuni inayouza madawa ya kilimo basi moja kwa moja nita wafahamisha wasikilizaji wangu.

Hata kama nina ujuzi ninajua kazi yangu ni kukusanya uziefu na maarifa na kusambaza kwa wasiilizaji

Muda mwingine ninaweza kuanzisha mada tata ili kuanzisha majadiliano tu.ili kupata taarifa kamili, Nitajitahidi kukaa mbali na majadiliano na kuwaacha wasikilizaji wachangie maoni yao. Kwa mfano nikiwa na majadiliano na waziri wa afya, Nina weza, “Unaniambia kwamba kama mimi ni msichana mdogo na nina sikia maumivu katika maeneo ya siri,”hakuna unachoweza kufanya?”

Uadilifu inamaanisha kuwa, sito waambia tu wasikilizaji kile ninachokijua, ila pia kile ambacho sikijui. Kwa mfano, kama nitakuwa nikifnya simulizi juu ya kisima kilicho na sumu, nitaawambia wasikilizaji ni kiasi gani cha visima vimeathiriwa, na chochote ambacho wanastahili kujua. Lakini pia nitawaambia wasikilizaji kuwa sijui chanzo cha sumu ni nini na sijui kama sumu ina sambazwa na nini, nita wafaamisha wasikilizaji kuwa bado nina fanyia kazi simulizi.

Uadilifu wangu na usawa utaonekeana Zaidi hasa katika mada zinazo gusa hisia za mtu, hasa hasa pale umbea na uongo unapokaribia kukubalika kama ukweli. Kwa mfano, kuna taarifa mtaani zinazuka kuwa kula viazi lishe kunasaidia kuponya matatizo ya macho. Taarifa zingine za uzushi ni zile kuwa aina Fulani ya mihogo inasababaisha kensa

Muda mwingne siwezi kumpata mtu atakaye simamaia upande mmoja wa simulizi tata. Kwa namna hiyo, Nitawajulisha wasikilizaji wangu wajue maamuzi niliyo chukua kujaribu kumtafuta mtu wa namna hiyo, na nitaendelea kujaribu.

Pia nitaelezea kwanini mtu aliyehojiwa kwanini hayupo kwenye kipindi. Na muda huo ikiwa kuwa “Waziri X hata taka kuhojiwa katika kipindi chetu,” inaonyesha uadilifu na haki kuongeza: “kwaababu atahudhuria harusi ya binti yake.”

Ni vigumu kwa wageni wangu kusahau kuwa walipaswa kufanya mahojiano katika kipindi changu.Nitaendelea kujitahidi kuwapigia wageni wangu simu, Nitawafahamisha wasikilizaji wangu kuwa nitaendelea kuwahoji wageni.

Baada ya, kuongea na wakulima, kituo change cha redio na kipindi changu kinaweza kuchukua nafasi katika kipindi cha kilimo. Kwa mfano kituo change cha redio kinaweza kuamua kipindi kizungumzie juu ya mbinu Fulani za kilimo kama namna ya kuhifadhi mahindi yasiliwe na wadudu. Kwa hali kama hii, Kwa hali kama hii nitawajulisha wasiilizaji sababu ya kituo kuchukua hatua hii. Lakini bado nitaendelea kutoa maoni mbalimbali juu ya aina hiyo ya kipindi.

Heshimu

Nina waheshimu wasikilizaji wanao zalisha chakula kwa familia yao na jamii kwa ujumla, Nina heshimu utofauti wa maarifa katika jamii yangu na sionyeshi utofauti wa kijinsia, umri,kabila au utofauti wa kiimani.

Mahusiano yangu na wasiilizaji wa vipindi ni wa dhamani. Imejengwa kwa makubaliano ambayo hayajatamkwa wala kuandikwa nina kuubali kuendesha vipindi ambavyo ni vya haki, usawa, vya manufaa, na vina taarifa husika. Nitaonyesha heshima hii kwa kutoa aina mbali mabli na maoni mbali mbali ya wasikilizaji na kuwa tayari kusikia maoni mbalimbali na kutoonyesha ubaguzi.

Nina waheshimu wachangiaji katika kipindi na wasikilizaji wote sawa. Wanajua kwanini wamealikwa katika kipindi na kuwapa muda wa kujiandaa ili kujua nini watakachoongea katika kipindi.Kama mtangazaji nitauliza maswali ya kudadisi kuwakilisha mawazo ya wasiilizaji wangu na wakati huo pia nikitunza mahusiano ya wageni waalikwa studio

Kila mtu anafahya makosa. Ninapo fanya makosa hewani, Nitakubali mara moja, hii ni sehemu ya heshima kwa wasikilizaji wangu

Mtu atakapotoa malalamiko juu ya kipindi change nita fanyia kazi malalamiko mara moja, Kama malalamiko ni makubwa nita fikisha ujumbe moja kwa moja kwa uongozi

Wapi kwingine ninaweza kujifunza juu ya viwango vya uandishi?

Umoja wa utangazaji wa kiingereza. Miongozo. http://www.bbc.co.uk/editorialguidelines/guidelines
Umoja wa watangazaji Kanada. Viwango vya waandishi wa habari na vitendo. http://www.cbc.radio-canada.ca/en/reporting-to-canadians/acts-and-policies/programming/journalism/
Redio ya Taifa (NPR). NPR kitabu cha maadili. http://ethics.npr.org/
Ushirika wa utangazaji wa Australia, 2011. ABC Sera za uhariri—Viwango. http://about.abc.net.au/wp-content/uploads/2015/09/EdPols2015.pdf

Shukrani

Imechangiwa na: Liz Hughes. Liz Hughes ana miaka Zaidi ya 40 katika kuchapisha, kurusha taarifa redioni,televisheni, na Makala ya mitandaoni, mzalishaji, mhariri mkuu na kiongozi nchini Kanada. Ni mwanachama wa bodi ya FRI

Kwa mchango wa Doug Ward, Mwenyekiti wa Bodi, FRI; Sylvie Harrison, Kiongozi wa timu ya redio, FRI; Vijay Cuddeford, Mhariri mkuu, FRI; Kevin Perkins, Mkurugenzi mtendaji, FRI; Edwin Kumah Drah, FRI Ofisa redio Ghana; na Rosemary Gaisie, Ghana Umoja wa watangazaji Ghana na mkufunzi FRI.

The translation of this resource was made possible with the support of USAID’s New Alliance ICT Extension Challenge Fund, through the International Fund for Agricultural Development in Tanzania. For more information about the Fund, please see: https://www.ifad.org/

Mradi umefanyika na ufadhili wa kutoka serikali ya Kanada kupitia kitengo cha mahusiano ya mambo ya nje(GAC)