Viwango wastani (F.A.I.R.) vya watangazaji kwa vipindi vya ukulima

Utangulizi

Katika mwaka wa elfu mbili na nane, kampuni ya Farm Radio International ilianzisha viwango vya vipindi vilivyorekodiwa. Viwango hivi husaindia watangazaji kuzalisha vipindi vinavyotoa mafunzo mwafaka, kupatia wakulima nafasi ya kutoa maoni yao na kuvutia umati mkubwa wa wasikilizaji. FRI pia iliwasilisha orodha ya mambo ambayo watangazaji wanafaa kufuatilia ili kujua umuhimu wa vipindi vyao kwa wasikilizaji kwa kutumia viwango hivyo.
Watangazaji wa kilimo pia wanafaa kuafikia viwango vya watangazaji. Watangazaji huhudumia wasikilizaji vizuri zaidi kupitia vipindi vya redio wakati wanapozungumzia kuhusu ujumbe ulio sahihi na mada inayoeleweka. Kwa mfano - wakati wa kupanda, jinsi ya kuchanganya mbolea, na mtu wa kupigia simu iwapo kuna changamoto fulani. Watangazaji pia huhudumia wasilizaji vizuri zaidi wanapowasilisha pande zote za swala lenye utata. Wasikilizaji huzawadi stesheni - ya redio inayoaminika- inayotoa ujumbe sahihi na mtazamo mbali mbali - wa mawazo kwa uaminifu.
FRI ina lengo la kusaindia watangazaji kupata kuaminiwa na wasikilizaji. Ndio sababu tunawasilisha viwango wastani vya F.A.I.R. kwa vipindi vya wakulima. Tunatumaini kuwa watangazaji watapata ujumbe huu ukiwa wa muhimu. Tunawaomba kutoa maoni yenu kuhusu viwango vya F.A.I.R ili tuweze kuviimarisha baada ya muda fulani kila wakati. Tafadhali tuma maoni yako kwa radio@farmradio.org.

Viwango vya F.A.I.R. kwa watangazaji wa kilimo kwa ufupi

Vifuatavyo ni viwango na semi ambavyo mtangazaji wa kilimo anapaswa kusema wakati wa utendakazi wao.

Haki na usawa: Hadithi zangu ni za haki na ziko na usawa. Ninawasilisha mitazamo mbali mbali na ninaheshimu haki za wasikilizaji kusikiza hadithi zangu kutoka pande zote.

Usahihi: Ujumbe ninaotangaza ni wa ukweli kutokana na utafiti. Ninawasilisha ukweli mtupu na pale kuna maoni ninaweka wazi au mtazamo na huyaweka sahihi.

Uadilifu: Ninafanya kazi kwa uadilifu wa kipekee na huwa siegemei upande wowote kwa maswala haswa wakati ni swala tata. Nikiegemea upande wowote, itaibua mjadala. Iwapo kuna kitu cha kibinafsi ninachoona kwenye swala fulani, hukifanya kujulikana wakati ninapepelusha kipindi. Na iwapo stedheni ya redio ikon a jawabu kuhusu swala fulani, ninafanya wasikilizaji kujua nikiwa hewani.

Heshima: Ninaheshimu wasikilizaji wanazalisha chakula kwa jamii zao na kwa watu wengine kwa mazingira magumu. Ninaheshimu aina mbali mbali ya wasikilizaji wangu na huwa sibagui kwa misingi ya jinsia, rangi, umri, dini, kabila, mila, tamaduni au vinginevyo. Ninaheshimu wageni wote na wanaochangia na vipindi vyangu hudhiirisha heshima kubwa kwa wasikilizaji wangu.

Haki na usawa

Hadithi na vipindi vyangu huwa vina haki nan a usawa. Ninawasilisha aina mbali mbali ya mawazo na ninaheshimu haki ya wasikilizaji kusikiza kutoka kwa pande zote mbili.

Haki na usawa huwa ni chanzo cha ujumbe wowote mzuri, vipindi na matangazo. Wasikilizaji wangu wanatarajia hili na wanataka kujua kila ujumbe utakaowafaa na mitazamo mbali mbali haswa kuhusu maswala tata na yaliyo na umuhimu. Kwa ujumla, mtangazaji mzuri wa ukulima huwasilisha pande zote za hadithi tata kwa njia ya haki na iliyokamilika inayowaruhusu wasikilizaji kufanya maamuzi yao.
Hata hivyo, huwa ni vigumu kuafikia usawa kwa kipindi kimoja kwa sababu ya muda haba, ukosefu wa wageni waheshimiwa na maswala mengine. Inapokuwa hivyo, tangazaji huafikia usawa kwenye baadhi ya vipindi – pande moja inaweza wakilisha pande ingine na pande inayofuata kuwakilisha pande tofauti.
Kuwa na haki pia humaanisha ninatia moyo mgeni aliyealikwa na aliye na ujumbe muhimu kwenye hadithi ila hukosa kujuhisi nyumbani wakiwa kwenye redio ama hawajazoea kuulizwa maswali kuhusu maoni yao.

Ni wajibu wangu kulinda maoni ya wanaoamini kuwa wanaweza kudhurika iwapo watafichua ujumbe fulani. Katika mfano huu, nitaficha jina la anayezungumza. Hata hivyo, nitahakikisha kuwa amepasha ujumbe wake kwa wasikilizaji na ombi lao la kutaka kutowekwa wazi kuzingatiwa. Haya yanapojiri, nitajadili swala hilo na mtu mwingine kwenye stesheni anayeaminika zaidi na anayetegemewa na anaye na uadilifu kama mwanahabari kabla ya kufanya maamuzi.

Nitakuwa na umakini ninapotangaza maoni tofauti yanayoweza kuwa na mvuto mkali haswa yale wanayoweza kuchochea chuki kwa mtu ama kikundi cha watu, ama kuzua vita. Hakuna nafasi ya hayo kwenye vipindi vya wakulima vilivyo na haki na usawa. Ni vibaya kufahamu kuwa redio inaweza kuchangia pakubwa kuzua chuki na vita na wengi hujaribiwa kufanya hivyo. Aina kama hii ya utangazaji huwa imekiuka viwangi vya F.A.I.R vya utangazaji. Iwapo mgeni katika redio atazungumza jambo ambalo huweza kuchangia chuki ama vita, sitakubali hilo lipite bila kuangaziwa. Nitampa changamoto na iwapo hatakubali kuomba msamaha na kuacha uchochezi, nitalazimika kukatisha mahojiano.

Wakati nitakuwa makini kupeana muda wa maoni, nitaangazia kutafuta muda kwenye kipindi change kueleza chanzo cha chuki na vita.

Kuwa wakati ambapo haki na usawa hulazimika kuangaziwa kwa undani zaidi, haswa wakati wa uchaguzi. Kwa mfano, kunaweza kuwa na swala muhimu la ukulima katika kampeni za uchaguzi, na wagombeaji mbali mbali wanaweza kuwa na maoni tofauti ya kutatua swala hilo. Ninafaa kuwasilisha maoni hayo na ahadi zao kwa njia ya usawa. Iwapo stesheni yangi ni ya mtu kwenye ofisi ya serikali ama wa chama fulani, ninafaa kueleza wakulima wafahamu hilo.

Haki nausawa huhitaji kufanya hukumu na maamuzi. Kwa mfano, kunaweza kuwa na wagombea wawili ama watatu wenye haki sawa ya kuchukua mamlaka baada ya uchaguzi. Kunaweza kuwa pia na wagombea wengine watano ama sita ambao hawana uwezo wa kushinda baada ya uchaguzi. Ninafaa nitumie maamuzi yamgu mazuri kujua nitapatia muda gani kwa wenye uwezo wa kushinda na wasio na uwezo wa kushinda. Kwa ajili ya wasikilizaji wangu, nitaangazia kwa kipana wagombeaji walio na uwezo wa kushinda bila kusahau wale wasio na uwezo wa kushinda pia.

Ninafaa pia kuonyesha haki na usawa na kufanya maamuzi vizuri kwenye vipindi vinavyohusisha kupokea simu na hamojiano mafupi yaliyorekodiwa. Ni vizuri kusikia maoni ya wasikilizaji kwa uwazi. Lakini ni vizuri kujua kuwa mazungumzo ya simu na mahojiano mafupi yaliyorekodiwa sio utafiti wa kisayansi. I wapo wakati wa kupokea simu wasikilizaji watano watatoa maoni sawa, haimaanishi kuwa kila mmoja ako na sehemu ya mawazo hayo.

Inamaanisha kuwa watu watano ambao wamepiga simu kwa wakati huo wana mtazamo unaofanana. Waliopiga simu wanaweza kuwa watu wenye utajiri wa kupita wastani, wasomi na wanaume. (Hawa ndio watu wanaohusika kwenye upigaji wa simu kwa mara nyingi). Nitajizatiti kufikia watu ambao hawana uwezo wa kupiga simu mara kwa mara kwa mfano kupitia kuwatembelea kwenye nyanja mbali mbali wanazoishi ama kufanyia kazi.

Iwapo swala linalowafanya watu kupiga simu ni la muhimu ama la kukanganya, na wanaopiga simu hawatoi mawazo mapana kuhusu swala hilo, nitatafuta njia mbadala za kuelezea upande mwengine wa swala hilo kwenye vipindi vingine.

Ninapofanya kila niwezalo kuafikia haki na usawa, ninafanya kazi kwa vipindi vya redio vinavyopiga jeki mtazamo wa wakulima wadogo wadogo na jinsi ya kuishi maisha ya afya mashinani. Hata hivyo, upigaji jeki huo huhusisha mitazamo mbali mbali kuhusu maswala muhimu kwa wakulima wadogo wadogo na wananchi wanaoishi mashinani.

Usahihi

Ujumbe ninaotangaza ni wa ukweli kutokana na utafiti. Ninawasilisha dhibitisho zote na ninaweka wazi kama jawabi ni maoni, mtazamo wa kimawazo na kama ni ukweli au la.

Ukweli ni muhimu. Huwa nafanya utafiti kuhakiksha kuwa ninatangaza mambo yaliyo muhimu zaidi na hoja zenye faida. Kwa mfano, kwenye ripoti zangu za hali ya anga na za soko, huwa nachunguza kuangali kuwa ujumbe ninaotoa ni sahihi na wa hivi karibuni kama iwezekanavyo na unakuja na vyanzo vya kueleweka na kuaminika. (Kama ujumbe sio sahihi na umepitwa na wakati, ninajua kuwa utakuwa na adhari mbaya kwa na kipindi change kinaweza kukosa kuaminika na wasikilizaji, pamoja na stesheni ya redio ninayotumia kupeperusha vipindi.
Ninapokusanya ujumbe kutoka kwa mtu mwengine, ninatumia maamuzi yangu na kufanya utafiti kama inavyohitajika ili kubaini iwapo uchunguzi wa mtu ni sahihi au la.

Kila inapowezekana, nitasema pale nimetoa ujumbe fulani ninaopeana kisha nitaje vyanzo vya ujumbe wangu.

Kwa mfano, nikiangazia hadithi kuhusu maandamano ya wakulima wakitaha haki itekelezwe kuhusu kuboresha barabara, sitasema kuwa kulikuwa na waandamanaji kia mbili kama sikuwa hapo nifanye hesabu yao ama mtu ninayemwamini alikuwa hapo akafanya hesabu ya kuaminika. Badala yake, nitasema kuwa “Kulingana na utafiti, kulikuwa na waandamanaji mia mbili” ama bora zaidi niseme “waliokuwa wakifanya mipango ya maandamano waliweka nambari ya watu mia mbili”, iwapo ni waandamanaji wananipatia nambari hizo.

Hakuna kitu muhimu zaidi cha kuzungumza ukweli kando na kusema nilikuwa hapo na haya ndiyo matokea niliona na kupata.

Ukweli ni rafiki zangu. Wao hupatia hadithi zangu na vipindi vyangu uaminifu na athari nzuri. Kwa mfano, kama ninaenda kufanya hadithi kuhusu jinsi mabadiliko ya hali ya anga yanaathiri majira ya kupanda kwa wakulima wadogo wadogo, ningesema kwa urahisi kuwa “majira ya kupanda yameadhiriwa na mabadiliko ya hali ya anga kwa muda wa miezi kumi iliyopita”. Lakini ingekuwa tata zaidi kusema kuwa kwa miaka kumi iliyopita takwimu za anga zinaonyesha kushuka kwa asilimia arubaini ya mvua kwa eneo hili, na kipindi cha upandi kimefupishwa kwa miezi miwili.

Nitakabiliana kwa umakini na mila na tamaduni zinazoshikiliwa na wakaazi. Kwa mfano, kumekuwa na tetezi nyingi kuhusu tiba ya ugonya wa ukimwi na virusi vya HIV kwa miaka mingi iliyopita, na tetezi hizo zimeaminiwa kwa wingi na baadhi ya wakkazi. Mfano mwingin ni; wakulima wengine huamini kuwa kuchoma mabaki ya chakula ni muhimu kwa kutoa mbolea na kufanya mchanga kuwa na totuba. Na kuna dhibitisho kuw hii ni kweli. Lakini tafiti nyingi za kisayansi zinasema kuwa kuchoma mabaki ya chakula huadhiri pakubwa rotuba ya mchanga. Mfano mwingine; Kuna aina mpya ya mihogo inayostahimili kiangazi inayoweza kusaindia wakulima wa nchi ya Uganda kudhibiti baadhi ya magonjwa. Kwa njia nyingine, minong’ono yasema kuwa aina hii mpya ya mhogo inaleta ugonjwa wa saratani. Minong’ono hii ilikuwa ya uongo lakini ilizambaa kwa mapana. Ili kuafikia malengo yaliyowekwa ya wanahabari, stesheni ya redio inayopeperusha kipindi cha aina hii ya mihogo inafaa kutumia ukweli na dhibitisho ili kupatia changamoto mila hii potovu kuwa aina hii ya mhogo huleta saratani.

Nitasaindia marafiki zangu kuelewa tofauti kati ya ukweli na maoni kwenye maswala muhimu. Maoni ni ya kudhaminiwa na huchangia pakubwa kwa program za ukulima. Maoni husaindia kueleza jinsi mtu binafsi ama kikundi cha watu kinavyochukulia swala fulani na hatua watakazochukua kutoka kwazo. Hata hivyo, ni wajibu wangu wa kwanza kuhakikisha kuwa wasikilizaji wamejua mambo ya muhimu na wajue kuainisha na mambo mengine.

Kwa nyakati kama hizi, nitaangazia ukweli, nitafute nasaha kutoka kwa wataalamu, na nitaje minong’ono kama hiyo ambayo siyo ya kweli. Ndio maana baada ya kufanya utafiti kuhusu swala hili, ninaweza kusema kuwa dhibitisho linaloweza kutegemewa zaidi linasema kuwa kuchoma mabaki ya chakula hupunguza nguvu na rotuba ya mchanga na hupunguza uzalishaji wa vyakula kwa muda mrefu. Lakini nitasema haya kwa njia inayoonyesha heshima kwa wasikilizaji. Wanafaa ujumbe unaopatikana lakini hawafai kujuhisi kana kwamba ninawahukumu.
Nitajikumbusha kuwa wataalamu wanasema kile wao na marafiki zao wa kilimo wamepata kuwa kweli kwa mara nyingi. Wanaweza pia kutoa maoni yao ama maoni ya biashara na serikali inayowaajiri. Kwa wakati unaofaa, nitauliza wataalamu kudhibitisha matamshi yao.

Kutoa maamuzi kwa kuangalia kitu bila kudhibitisha ndiyo shida kubwa. Kwa mfano watu wengi huamini kuwa wafugaji wa ngombe wa kuhama hama kutoka Africa magharibi ni wa jamii ya Fulani, na jamii hiyo ya Fulani huleta shida kwa wakulima wadogo wadogo. Jamii ya Fulani na mifugo wao hulaumiwa kwa kila jambo baya linalotokea kwenye eneo la mkasa ikiwemo kubakwa kwa watu kwenye shamba, wezi wa kimabavu kwenye njia kuu, na uharibifu wa kukusudia au wa kibahati mbaya wa mimea. Haya ni baadhi ya mambo wanayoamini ambayo sio ya haki na ni mabaya. Ni muhimu kuepuka mambo kama haya haswa kwa mtu ama kikundi cha watu kufuatilia kabila, tamaduni, kidini na mengineyo. Wakati ninapotoa hotuba, nitabakia kusema ukweli mtupu kama ninavyjua na niwe na umakinifu kuepuka kutoa hukumu nisizojua wala kufahamu au kudhibitisha.

Nitasaindia wasikilizaji kuelewa tofauti kati y ukweli, maoni na maswala mengine yenye umuhimu. Maoni yanadhaminiwa na huchangia pakubwa kuleta matokea borawenye programu. Maoni huonyesha jinsi kundi la watu ama mtu binafsi hudhamini maswala mbali mbali na hatua wanazochukua kuhusu maswala hayo. Hata ivyo, ni wajimu wangu kuhakikisha kuwa waikilzaji wnajua maswala muhimu, n kuwianisha n ukweli unaojitokeza kutoka kway.

Nitatoa changamoto na nipiganie kuzungumza ukweli katika mahojiano. Kama anayewakilisha wasikilizaji wangu, nitauliza maswali ambayo wakulima wangeuliza kwa niaba yao. Kwa hivyo kampuni inayoshughulikia uzalishaji kwa mbegu ikidai kuwa aina fulani ya mbegu hutoa mazao maradufu, nitadai dhibitisho la madai hayo. Iwapo mmoja wa wafanyikazi wakuu atasema kuwa aina mpya ama namna mpya ya upaliliaji huongeza mazao kwenye mashamba ya wakulima, nitaomba watoe dhibitisho ili kubaini ukweli wa semi zao.

Udailifu

Vitendo vyangu vyote vinaonyesha uadilifu wa kibinafsi na ni nadra kuegemea upande mmoja kwa maswala muhimu haswa wakati swala ni la kutatanisha. Iwapo nitaegemea upande mmoja, itakuwa tu ni kwa lengo la kuchangia mjadala uweze kushika kasi. Nikiegemea upande mmoja kwa swala lolote, ninafaa kutangaza hewani ili wakulima waweze kufahamu hilo. Na iwapo stesheni yangu ya redio ikon a msimamo kuhusu swala fulani, ninatangaza hewani pia kujulisha wasikilizaji.

Nitajizatiti kushikilia ama kutoshikilia upande wowote, kuwa sawa kwa makundi yote na kuwa na haki kwa vipindi vyote vya utangazaji. Nitafanya kazi kwa lengo la kufaidisha jamii, kutafuta ukweli, kuuripoti kwa uadilifu na niwe wa kujukumikia matendo yangu yote.

Nitakuwa na umakini iwapo niko na swala la kibinafsi kuhusu swala tata kwa sabau nisipofanya hivi nitakuwa mbinafsi na nionekane kupendelea upande mmoja. Kama kuna kitu kutoka kwangu kupitia utafiti ama historia ninachojua kinachokuwa na umuhimu kwa hoja hiyo, nitakisema wazi wazi. Kwa mfano, iwapo nilikuwa ninafanyia kazi kampuni inayouza mazao mapya ya ukulima, nitaelezea wakulima wangu. Kama dada yangu ama mtu ninaye na uhusiano naye, hata uwe uhusiano wa mbali anaongoza kundi linalopigania bei nzuri na soko nzuri kwa wakulima, nitataja hil pia.

Hata kama niko na maarifa kuhusu nyanda fulani, ninajua kuwa jukumu langu muhimu kama mtangazaji na mwenyeji wa kipindi ni kukusanya maoni na ukweli kutoka kwa watu wengine nan a niweze kuyapeperusha hewani.

Mara kwa mara, ninaweza kutaja msimamo wangu kuhusu swala tata kwa lengo la kusaindia mjadala kushika kasi na kufunua jumbe zaidi kutoka kwa watu kupitia mazungumzo. Kwa nyakati kama hizi, nitajaribu kujiweka kando kutokana na maoni. Kwa mfano, katika majadiliano na wa cliniki ya afya, ninaweza kusema “kwa hivyo unaniambia kuwa kama mimi ni msichana mdogo mwenye ‘uchungu mwingi chini ya kiuni’ hakuna jambo lolote unaweza kunisaindia nalo kwenye cliniki yako hii?” Hiiyo ni kweli?

Uadilifu unamaanisha kuwa sitaambia wasikilizaji ninalojua pekee lakini pia niwaambia kile sijui. Kwa mfano, kama ninafanya hadithi kuhusu visima vilivyotiwa sumu na kemikali, nitaeleza wasikilizaji nambari ya visima vilivyoadhirika na kitu kingine chochote wanachofaa kufahamishwa. Lakini nitaeleza wasikilizaji kuwa sijui chanzo chanzo cha uchafuzi huo na iwapo unaendelea au la. Nitaeleza wasikilizaji kuwa ninaendelea kufuatilia hadithi hiyo.

Uadilifu na kuaminika kwangu ni muhimu sana haswa kwa hadithi tata na zenye hisia pale minong’ono na masengenyo yanaweza kupita ukweli. Kwa mfano, kuna minong’ono ya uongo kuwa ukikula mchanganyiko wa viazi na machungwa unaweza kuimarisha uwezo wako wa kuona. Minong’ono ya aina nyengine inayoonekana kama ya kweli ni kuwa ni ile tulitaja hapo awali ya aina ya mihogo inayoleta saratani.

Kwa mara nyengine, sitaweza kupata mtu wa kuwasilisha hoja tata ya hadithi kwa upande mmoja. Hli likitokea, nitamfanya msikilizaji wangu ajue hatua ninayochukua kujaribu kupata mtu kama huyo na kuwa ninaendelea kumtafuta.
Nitaeleza sababu za mgeni aliyekuwa amekaribishwa kukosa kufika kwenye kipindi. Na wakati inaweza kuwa ukweli kusema kuwa “waziri fulani alisema hatahojiwa kwenye kipindi chetu”, inaonyesha uadilifu na ukweli kuongeza kuwa “kwa sababu anahudhuria harusi ya binti yake”.

Inaweza kuwa mgeni wetu amesahau kuwa alifaa kufika kwenye studio ili kufanya mazungumzo wakati huu. Nitachukua muda kabla ya kufanya mamuzi kuwa mgeni wetu hatakuja na niendelee kujaribu kumtafuta kwa kupiga simu. Kama hatashika simu zangu, nitaeleza wasikilizaji kuwa nitaendelea kujaribu kufanya mazungumzo na mgeni wetu.

Kwa mara kwa mara baada ya kuzungumza na wakulima wadogo wadogo, stesheni yangu ya redio na kipindi change kinaweza chukua nafasi ya mwelekeo fulani wa ukulima. Kwa mfano, stesheni yangu inaweza amua kutumia kipindi kupiga jeki aina moja ya namna ya ukulima kama kupanda mahidi na maharagwe kwa kuyabadilisha kila msimu, ama njia mwafaka ya kutengeneza mbolea, ama njia ya kuhifadhi mahidi ili wadudu wasiyaharibu. Nyakati kama hizi, nitambia wakulima tunachukua mwelekeo fulani na niwaeleze sababu ya kufanya hivyo. Kisha nitachagua kipindi ambacho kitatekeleza wajibu huo. Lakini nitaendelea kutoa mitazamo mbali mbali kuhusu aina hiyo ya zoezi hilo na mtazamo kuhusu kipindi hicho.

Heshima

Ninaheshimu msikilizaji anayezalisha chakula kwa jamii yake na kwa umma haswa chini ya mazingira magumu. Ninaheshimu uwazi wa wasikilizaji wangu na sitabagua kwa misingi ya jinsia, rangi, dini, umri, kabila, tamaduni, kile wanachoamini au kwa misingi yeyote.

Uhusiano wangu kati ya kipindi na wasikilizaji ni wakipekee, uliojenwa kwa kandarasi iliyoandikwa ama isiyoandikwa. Ninakubali kufanya kipindi kinachovutia, kilicho na umuhimu, chenye haki na wasikilizaji wangu wakubali kusikiliza na kuingiliana na pengine watoe maoni yao kuhusu walichisikia. Ni kandarasi ya kuwa na heshima kutoka kwa pande zote mbili. Ninaonyesha heshimahiyo kwa kuwasilisha hadithi za aina kadhaa, mawazo na kwa kutoegemea upande mmoja na kufunguka kimawazo na kutoa maoni yasiyojulikana na kila mtu.
Ninaheshimu wageni wangu na wanaochangia na kuwapa heshima wanayofaa. Wanajua wakati wamealikwa kwenye kipindi na kile walichoagizwa kuzungumzia ili wapate muda wa kujiandaa. Hii haimaanishi kuwa sitauliza wageni wangu maswali magumu. Nitafanya kinyume cha hilo. Kama anayewakilisha wasikilizaji wangu, nitauliza maswali yenye changamoto kwa niaba ya wasikilizaji wangu. Nitafanya hivyo nikiwa na heshima kwa mgeni wangu.

Muda kwa muda, kila mmoja hufanya makossa. Nikifanya makossa nikiwa hewani, nitakiri haraka iwezekanavyo. Hii inaonyesha heshima kwa wasikilizaji wangu na mojawapo ya kandarasi niliyotia sahihi na wasikilizaji wangu.

Iwapo mtu atalalamika kuhusu program yangu, nitatoa jawabu haraka iwezekanavyo. Kama malalamishi ni ya kuchukuliwa kwa uzito zaidi, nitazungumza na meneja wa stesheni ya redio yangu.

Ni wapi ninaweza kupata mafunzo zaidi kuhusu kiwango cha watangazaji?

The British Broadcasting Corporation, undated. Editorial Guidelines. http://www.bbc.co.uk/editorialguidelines/guidelines

The Canadian Broadcasting Corporation, undated. Journalistic Standards and Practices. http://www.cbc.radio-canada.ca/en/reporting-to-canadians/acts-and-policies/programming/journalism/

National Public Radio (NPR), undated. NPR ethics handbook. http://ethics.npr.org/

Australian Broadcasting Corporation, 2011. ABC Editorial Policies—Principles and Standards. http://about.abc.net.au/wp-content/uploads/2015/09/EdPols2015.pdf

Shukrani zifikie wafuatao

Imechangiwa na: Liz Hughes. Liz Hughes ambaye ako na zaidi ya miaka arubaini kwenye tajriba ya wachapishaji wa Canada wa magazeti, redio, televisheni, na vifaa vya kuandika kwenye mtandao kama mwanahabari, mchapishaji mkuu, mwenyekiti wa kutengeneza video na kiongozi mkuu. Yeye ni mwanakamati wa bodi ya viongozi ya FRI.

Imechangiwa na Doug Ward, mwenyekiti, bodi ya viongozi, FRI; Sylvie Harrison, mwelekezaji wa kikundi cha wanaredio, FRI; Vijay Cuddeford, Kiongozi wa ukarabati, FRI; Kevin Perkins, Kiongozi mteule, FRI; Edwin Kumah Drah, FRI afisa wa maswala ya redio, Ghana; na Rosemary Gaisie, anayetoa mafunzo kwenye kitua cha utangazaji, Ghana.

Mradi huu wa Canada umefanikiwa kutokana na ufadhili na kupiwa jeki kutoka serikali ya Canada na kupitia kundi la maswala ya nchi ya Canada (GAC)

This resource was translated with support from The Rockefeller Foundation through its YieldWise initiative.