Jinsi ya kuhudumia wakulima wa kike vizuri

Je, niko na wakulima wa jinsia ya kiume na ile ya kike pia?

Kwa miongo mingi iliyopita, vipindi vya redio vya wakulima vimekuwa vikitimiza mahitaji au kusaindia wakulima wa jinsia ya kiume pekee.
Watangazaji wa redio wa kiume wamekuwa wakifanya mahojiano na wataalamu wa kiume na wakulima wa jinsia ya kiume kuhusu mazao wanayopanda na mifugo wanayofuga.
Hii leo, tunafahamu kuwa wanawake hufanya kazi ya kilimo sawa na wanaume kwenye mashamba madogo madogo. Wao pia hulea jamii zao na kutunza watoto na waliozeeka.
Kwa hivyo wanawake wana umuhimu mkubwa kwa maisha ya wanajamii na mashamba kwa jumla. Hivyo basi ni muhimu vipindi vya redio vinavyokusudiwa kulenga wakulima wadogo wadogo vitimize mahitaji na maombi ya wakulima wa jinsia ya kike na ile ya kiume.

Mwongozo huu utanisaindiaje kuhudumia wasikilizaji wangu vizuri zaidi?

 • Wakulima wa jinsia ya kike watapata ujumbe wanaohitaji ili kufanya ukulima bora zaidi.
 • Wakulima wa jinsia ya kike watakuwa na uwezo wa kutoa maoni yao kwa maswala yaliyo muhimu kwao nay ale yanayowahusu.
 • Wakulima wa jinsia ya kike watafurahia vipindi zaidi.
 • Wakulima wa jinsia ya kiume watasoma zaidi kilicho na umuhimu kwa wanawake wa jinsia ya kike na wataweza kutilia maanani.

Mwongozo huu utanisaindiaje kuzalisha na kuwa na vipindi bora zaidi vya redio?

 • Inanipatia njia mwafaka kupitia vitendo zitakazoniwezesha kuvutia na kuhudumia wakulima wa jinsia ya kike wanaosikiliza vipindi na hivyo kusaindia kuinua kiwango cha wasikilizaji wangu.
 • Hunipa maoni jinsi ninavyoweza kutia moyo usawa wa kijinsia kwenye stesheni yangu ya redio.

Je, nitaanza vipi?

 1. Kwa kupatia wakulima wa jinsia ya kike heshima wanayostahili.
 2. Kufanya utafiti kuhusu mambo yanayowafaa wanawake na kisha kuyajadili.
 3. Kupeperusha vipindi kwenye redio watati mwafaka ambao wakulima wa jinsia ya kike wanaweza kupata nafasi ya kusikiliza.
 4. Kutia wakulima wa jinsia ya kike moyo na motisha ili waweze kuzangumza hewani vipindi vinapoendelea.
 5. Kuhakikisha kuwa stesheni yangu haibagui wasikilizaji kwa misingi ya kijinsia.

Ufafanuzi wa hoja kwa undani

1. Kupatia wakulima wa jinsia ya kike heshima wanayostahili

Kama ilivyotajwa hapo juu, wanawake ndio hufanya kazi nyingi kwenye ukulima wa mashamba madogo madogo. Na wanafanya hivi wakiwa na shughuli zingine nyingi kama kutunza watoto na waliozeeka. Kazi yao huchangia pakubwa kwenye maisha mora katika jamii. Kwa kila jambo unalofanya ikiwemo kuzalisha, kuhoji, ama kualika wageni kwenye studio, hakikisha kuwa unatambua na kuonyesha heshima kwa wanawake ambao hufanya bidii, hufanya maamuzi muhimu kwa kuonyesha kujali afya na hali ya familia zao licha ya kuzingirwa na watu wasiowaheshimu kwa sababu ya jinsia yao. Mwisho kabisa, hakikisha kuwa unatambua mambo mengi kama ya biashara na utangamano mzuri ambayao wanawake na wanaume huchangia katika jamii yao na katika maeneo wanayoishi.

Kwa mfano;

 • Tambua akina mama kama wakulima wala sio kama bibi ya wakulima.
 • Unapozungumza, tumia majina yao wala sio kuwaita wanawake kwa ujumla.
 • Uliza maoni yao kuhusu maswala muhimu ya ukulima. Utashangaa kujua kuwa kuna mengi wanayojua.
 • Toa mifano ya hadithi za ufanikishi kulingana na jinsia iliyofanikisha. Kwa mfano, wanawake huhusika katika kupanda mazao ama wanaume kuhusika katika kutoa maamuzi bora kuhusu afya kwa ajili ya jamii zao.

2. Fanya utafiti kuhusu mambo muhimu kwa wanawake na uyaangazie

Kulingana na tamaduni, tunafikiria kuwa ukulima ni kazi ngumu inayoweza kufanywa na wanaume pekee. Na kuwa wanawake hujishughulisha na mashamba ya mboga. Lakini ukweli ni kuwa wanawake wanajali na wanahusika kwa kila hatua ya ukulima inayoathiri afya ya jamii zao, ikiwemo kiwango na ubara wa wa mavuno.

Kwa mfano;

 • Jinsi ya kufanya mchanga uwe na rotuba nzuri
 • Muda unaofaa wa kuuza ng’ombe
 • Jinsi ya kuongeza lishe bora kwa mazao
 • Jinsi ya kuchukua mkopo kwa umakini ili kuongeza uzalishaji wa chakula
 • Jinsi ya kuweka akiba hadi zitakapohitajika na familia.
 • Enda kwenye kijiji na ufanye kikao na wanawake. Waulize ni maswala gani muhimu wanayokumbana nayo katika kazi yao ya ukulima. Pendekeza baadhi ya hoja zilizojadiliwa hapo juu ili wasifikirie tu kuhusu ukulima pekee. Sikiliza kwa makini na hatimaye wafahamishe hoja muhimu utakazozipa kipao mbele. Kisha ukirudi kwenye stesheni, fikiria jinsi utakavyoangazia maswala haya.

  3. Peperusha vipindi wakati mwafaka ambapo wakulimawa kike wataweza kusikiliza

  Unaweza kuwa na vipindi vizuri sana vinavyoweza kufaidi wakulima wa jinsia ya kike vizuri zaidi lakini ukivipeperusha wakati ambapo wanawake wengi hawako karibu na redio, utakuwa unafanya kazi bure. Wakati unapotembea kwenye vijiji, kutana na wanawake na uwaule wakati mwafaka ambao wanaweza kusikiza vipindi vya ukulima kwenye redio. Uliza wanaume swali hilo moja pia. Iwapo wakulima wote wa kike na kiume wanapatikana kwa wakati mmoja, unaweza kupeperusha kipindi kimoja kinachoangazia jinsia zote. Lakini iwapo wanawake hawawezi kusikiliza wakati sawa na wanaume, utalazimika kupeperusha kipindi chako mara mbili kwa wiki ili wakulima wa jinsia zote wapate kusikiliza. Bila shaka kipindi chako hicho kitakuwa tata haswa iwapo wasikilizaji watahitajika kupiga simu kwani watatakiwa kuwa hewani. Kwa swala kama hili, utastahili kurekodi na kisha kucheza mahojiano yaliyokuwa hewani kati yako na mkulima. Aidha, unaweza pia kuwa na vipindi viwili tofauti, kimoja kikilenga wanaume na kingine kikilenga wanawake.

  4. Kutia wakulima wa kike motisha wa kuzungumza hewani

  Kwenye tamaduni nyingi, wanawake hukosa kuzungumza na kuwapa wanaume muda wa kuzungumza kwa niaba yao, watoto wao na jamii zao. Lakini majira yanabadilika. Wanawake wana haki ya kujizungumzia. Na jamii zenu zitakuwa na afya na bora zaidi na ziweze kusonga mbele iwapo sauti za wanawake zitasikika na kuangaziwa sawa na za wanaume katika kujadili maswala muhimu. Fahamu ni wapi wanawake wana ujasiri wa kuzungumza, labda kwenye nyumba zao, kwenye mashamba, ama kwenye vikundi vya marafiki na uwatembelee hapo. Katika mwongozo huu, utapata mambo muhimu unayoweza kufanya ili kutia wanawake motisha waweze kuzungumza hewani.
  Kwa mfano;

  • Kutafuta wanawake walio na ujasiri kuzungumza hewani
  • Kuhoji wanawake kwenye makundi
  • Kukubali mwanamke kuzungumza kwa jumla kwenye mazingira mbali mbali

  5. Hakikisha kuwa stesheni yako haibagui wasikilizaji kwa misingi ya kijinsia

  Kuna njia njingi wasikilizaji wanaweza tambua kama stesheni yako ina ubaguzi kuhusian na jinsia au la. Pitia mwongozo huu;

  • Je, huwa unaalika wanawake kutembelea stesheni mchana wakati hawana tishio la kusafiri?
  • Je, uko na vyumba vya kutumia kwenda haja kwa wanawake na wasichana?
  • Je, kila mmoja kwenye stesheni yako anawapa wanaume na wanawake heshima wanayostahili?
  • Je, wasikilizaji wanasikia watangazaji wa jinsia ya kike wakifanya kazi ambayo watangazaji wa kiume wanafanya? (Stesheni nyingi za redio hazina rekodi nzuri za watangazaji wa kike kupeperusha vipindi hewani.)
  • Je, stesheni yako iko na mikakati ya kisheria ya usawa wa kijinsia? Mikakati hii inazingatiwa na kutiliwa maanani?

  Orodha nyengine ya mwongozo kuhusu kuhudumia wakulima wa jinsia ya kike vizuri

  Tumia laini tofauti ya kupiga simu na uitenge kwa wakulima wa kike pekee

  Wanawake huwa na ugumu wa kupata simu zaidi kuliko wanaume. Kwa hivyo ikiwa asilimia tisini ya wanaume wako na simu, inamaanisha kuwa asilimia 90 ya simu zitakazopiwa zitakuwa kutoka kwa wanaume. Lakini iwapo utatenga laini kando ya kutumika na akina mama pekee, unaweza kuwa unabadilisha laini hizo na asilimia hamsini ya watakaopiga watakuwa wanawake. Hata ingawa itakuwa gharama unapojaribu kuona kuwa wanawake wanapata nafsi ya kupiga simu, hii ndio mjia bora zaidi ya kufanya wanawake wajihisi kuwa maoni yao na mchango wao unadhaminiwa kwenye vipingi vya redio.

  Tafuta nafasi ukutane na wakulima wa jinsia ya kike

  Fanya mpango wa kupata nauli ili uweze kufikia maeneo ambayo kuna ukulima. Peperusha ziara yako hewani ili utakapofika upate watu wengi. Kama wewe ni mtangazaji wa kiume, fika studioni na mtangazaji wa kike. Hii itafanya wanawake wawe na ujasiri wa wa kuzungumza utakapokutana nao.

  Tafuta wanawake walio na ujasiri ya kuzungumza hewani

  Ukipata mwanamke ambaye ako na ujasiri wa kuzungumza hewani, na aliye na hoja na maoni muhimu, chukua namba yake ya simu ili uweze kuzungumza naye baadaye kuhusu hoja zengine tofauti. Hii itapatia wanawake wengine ujasiri wa kuzungumza kwenye vipindi vitakavyofuata.

  Fanya mahojiano na wanawake kwenye vikundi

  Ukifanya mahojiano na mwanamke mmoja pekee, hatakuwa na uhuru wa kuzungumza kwa sababu atakuona kama mtaalamu. Lakini ukihoji kundi la wanawake, kila kiyu hubadilika. Wanawake hupata nguvu na ujasiri wakiwa wengi. Na mwanamke mmoja akitoa wazo, mwengine anajihisi kuwa anaweza chambua hoja kwa undani n ahata atoa wazo boara zaidi. Kisha mwanamke wa tatu atatia nguvu yaliyojadiliwa na atoe mawazo bora zaidi kuliko wote.

  Patia wanawake walioko mashinani simu

  Kwa baadhi ya vivi, hakuna mwanamke anayemiliki simu. Kama unaweza kupata simu, patia mwanamke mmoja unayemwamini kisha wanawake wote wawe wakiitumia kupiga simu wakati kuna vipindi.

  Angazia maisha na uzoefu wa wakulima wa jinsia ya kike

  Sote tunahitaji kusikia kuhusu watu wanaofanana na sisi. Wenzetu wanapambana vipi na changamoto kama zile tunapitia? Nini huwapa raha au huzuni? Fanya mahojiano na wakulima wa jinsia ya kike na waeleze mapiti yao hewani. Hii itatia moyo wanawake wanaopitia changamoto sawa na hizo.

  Ungana na kundi la akina mama

  Tafuta kikundi cha akina mama na uwaalike kusikiza kipindi chako na utoe maoni kuhusu vile kipindi chako kitakidhi mahitaji yao. Kwa maelezo zaidi kuhusu vikundi vya wanaosikiliza, tafadhali bonyeza hapa.

  Tumia maneno ya akina mama ya ukulima

  Katika maeneo mbali mbali, wanawake wako na maneno ya kilimo yanayoeleza mazao fulani au njia fulani ya ukulima. Maneno haya huwa hayajafahamika na wakulima wa kiume ama wataalamu wa kiume au hata wakulima wa kiume. Tumia maneno mabayo wakulima wa jinsia ya kike hutumia na kuekewa.

  Kubali mwanamke azungumze bila kujitambulisha ama kutaja yeyote kwa wakati specieli

  Kama mwanamko anapitia mateso fulani nyumbani kwake ama kwenye ameneo ya kazi na anaogopa matokeo iwapo atatambulika kuwa ndiye aliyesimulia hadithi fulani kwa kipindi chako, msaindie kusimulia hadithi yake kwa wasikilizaji. Kama unajua mwanamke, jina lake na unajua hadithi yake ni ya kweli, hauna haja ya kutangaza jina lake ama kujaribu kumhusisha na hadithi aliyosimulia. Unaweza kujaribu kuficha sauti yake kwa kuiharakisha ama kuifanya kucheza pole pole kwa kutumia kompyuta. Ama unaweza kusimulia hadithi yake bila kumtaja. Utagundua kuwa kwa kusimulia hadithi yake, utasaindia wanawake wengine wengi walio na mapito sawa maishani. Hiyo itawasaindia na itakusaindia wewe kama mtangazaji kuanza kuzungumzia maswala mengine fiche kutokana na hadithi kw undani. Kumbuka kuwa kuficha sauti yake na jina lake pekee haitoshi. Karibu kwa vyovyote vile kuficha ujumbe wowote unaoweza kumfanya kutambulika.

  Wakilima wa jinsia ya kike ni wataalamu pia

  Kuna baadhi wa wakulima wa kike ambao wanajua mengi kuhusu kilimo kama wataalamu unaohoji kwenye stesheni. Fanya mahojiano na wanawake wa aina hii hewani. Ujumbe wao utakuwa na umuhimu mkubwa kwa wakulima na mfano wao utasaindia wanawake wote kuelewa kuwa wanawake wana umuhimu kwenye ukulima.

  Badilisha jinsi unavyofanya mahojiano yako kwa wakulima wa kike na wale wa kiume

  Iwapo mtaalamu atazungumzia kuhusu umuhimu wa kudunga ng’ombe sindano ili kuzui magonjwa kwa manufaa ya mkulima wa kiume, muulize jinsi hatua hiyo itasaindia mkulima wa kike na familia nzima kwa jumla. Na hakikisha umebaini kuwa dawa hizo za kukinga maradhi zinaweza kupatikana na wanawake kama zinavyopatikana na wanaume.

  Usizungumze na wanawake kuhusu mazao ya shambani pekee

  Ni kweli kuwa wanawake wengi hufanya kazi nyingi za jikoni na za shambani. Lakini wanapendezwa na ukulima wote jamii inayojihusisha nao. Na watakuwa na mawazo kuhusu muda mzuri wa kuuza ng’ombe, chakula ama njia bora ya kuongeza rotuba kwenye mchanga ama iwapo ni vizuri kuchukua mkopo kupata bidhaa za shambani.

  Funza wakulima jinzi ya kutumia simu

  Baadhi ya wnawake hawajapata nafasi ya nkusoma kuhusu namba shuleni. Hata kama wanamiliki simu, hawajui nuweka nambari sahihi. Wafunze njia rahisi ya kutumia nambari hizo kwa njia rahisi nay a kueleweka. Fanya jaribio ukitumia mwanamke mmoja ili ujue iwapo inasaindia.Kama inasaidia, itangaze hewani mara kwa mara.

  Ifuatayo ni njia mojawapo ya kusaindia wasikilizaji kuelewa zaidi kuhusu utumiaji wa simu. Unaweza kupata njia bora zaidi ya hii. Pengine simu yako ikon a njia mwafaka ya kukusaindia kukumbuka taratibu fulani. Cheza utaratibu huu wakati wa mapumziko kila wiki. Uliza akina mama iwapo inawasaindia.

  Kwa kutumia simu yako unaweza kuzungumza na ulimwengu mzima Unaweza kuzungumza na ulimwengu mzima
  Unafaa tu kufahamu
  Mahali sawa pa kubonyeza
  Kutoka kushoto kwenda kulia zinafuata hivi;
  - Laini ya kwanza – moja mbili tatu
  - Inayofutata nne tano sita
  - Ya tatu – saba nane tisa
  - Ya chini- sufuri

  Burudika unapokuwa hewani

  Kumbuka kuwa vipindi vinavyoburudisha na kuelimisha huwa bora zaidi kwa wasikilizaji wako. Tafuta njia ya kutumia hadithi za kitambo na za kisasa pamoja na nyimbo katika vipindi vyako.

  Furahia matunda yako

  Kila siku, wakulima wa jinsia ya kike wanafaulu baada ya kukabiliana na changamoto na wanapata mapato mazuri kwenye kilimo. Tafuta hadithi nzuri kama hizo za wanavyong’ara na uweze kuzifurahia.

  Ni wapi pengine ninaweza kusoma kuhusu kuhudumia wakulima wa jinsia ya kike vizuri zaidi kupitia vipindi vya redio?

  Adamou Mahamane, Fatouma Déla Sidi, and Alice Van der Elstraeten. 2014. Guidelines for the production of gender responsive radio broadcasts . Food and Agriculture Organization of the United Nations. http://www.fao.org/3/a-aq230e.pdf

  Ufafunuzi

  Kupatia wakulima wote wanachohitaji bila ubaguzi wa jinsia: Inamaanisha kuwa wanaume na wanawake wanapewa haki zao kwa usawa huku wakiheshimiwa kulingana na jinsia zao. Inafaa kuchukua hatua fulani ili kuafikia hili bila kuonyesha upendeleo. Kwa mfano; kutenga simu fulani kutumiwa na wanawake pekee ama kuangazia muda ambao wanawake wanapatikana kabla ya kupeperusha kipindi inalenga kuhakikisha kuwa jinsia zote zimewakilishwa sawa.

  Kuzingatia usawa bila kubagua kwa misingi ya jinsia: Inamaanisha kuwa wanwake na wanaume wanafurahia haki sawa, nafasi sawa na matukio katika maisha hayawekwi kwa msimgi ya jinsia. Inalenga kuhakikisha kuwa mahitaji, maoni, mapendekezo ya wanaume na wanawake yanabebwa kwa mizani moja. Kwa mfano, wanawake na wanaume wana haki sawa ya kupata ajira, kupandishwa cheo kazini, mazingira sawa ya utendakazi, mishahara na mengineyo. Usawa wa jinsia huhusiana sana na tabaka, umri, kabila, mwelekeo wa jinsia na juhudi za kupata usawa kwenye maeneo haya.

  Kuchukua hatua kwa misingi ya junsia: Inamaanisha kuchukua hatua ili kurekebisha kuegememea kwa jinsia moja ama kubagua jinsia moja ili kuafikia usawa. Inamaanisha kuwa utaangazia jnsia zote ili zikuongoze kwenye upeperushaji wa vipindi vyako. Huhusisha kuangazia maswala ya wanaume na wanawake na mahitaji yao huku ukizingingatia usawa kwa kila pande.

  Tunatambua wafuatao

  Waliochangia : Doug Ward, na ongezeko la vitabu kutoka kwa Caroline Montpetit, Sylvie Harrison, na Vijay Cuddeford

  Mradi huu wa Canada umefanikiwa kutokana na ufadhili na kupiwa jeki kutoka serikali ya Canada na kupitia kundi la maswala ya nchi ya Canada (GAC)

  This resource was translated with support from The Rockefeller Foundation through its YieldWise initiative.