Kufanya kazi kwa kuzingatia umbali kama mtangazaji wa redio

Wakati mwingine, watangazaji wa redio hawawezi kuripoti habari kwenye eneo la tukio au kwa kukutana uso kwa uso na watu wanaohusika. Hii ni kweli hasa wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) wakati serikali ulimwenguni kote zimetunga sera ambazo zinahitaji watu kuweka umbali wa mita moja kutoka kwa kila mtu isipokuwa wale wa nyumbani kwao ili kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi.

Lakini vyombo vya habari vinachukuliwa kuwa huduma muhimu katika nchi nyingi, na hii inamaanisha kuwa watangazaji wa redio watahitaji kuchukua njia stahiki na salama za kuendelea kuripoti, lakini kwa kuzingatia umbali.

"Huduma muhimu" ni zipi na zinahusianaje na matangazo ya redio?

Serikali tofauti zinaweza kuwa na vigezo tofauti vya kuamua ni huduma gani ni muhimu, lakini huduma muhimu kawaida zitajumuisha huduma za afya, chakula na kilimo, utekelezaji wa sheria, huduma zingine za rejareja, na biashara zingine ambazo ni muhimu kabisa kwa maisha ya kila siku. Utangazaji unachukuliwa kuwa huduma muhimu katika nchi nyingi kwasababu ni muhimu watu wapate habari sahihi na za sasa kupitia redio, Runinga, mtandao, machapisho, na njia zingine za kupata habari. Hii inamaanisha kuwa jukumu la vituo vya redio na watangazaji wa redio kutoa habari kwa wakati sahihi na habari sahihi ambayo ni muhimu kwa wakulima wa kiume na wa kike wa Kiafrika na familia zao ni muhimu zaidi kuliko hapo awali.

Kujifunza zaidi kuhusu jinsi watangazaji wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi wakati wa dharura, soma andiko la FRI- Matangazo ya jinsi ya kuuongoza katika kupanga na kutoa majibu madhubuti ya dharura kwa wakulima, na Mwongozo kwa Waandishi yetu juu ya kukaa salama kama mtangazaji wakati wa janga la ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).

Ni changamoto gani za kufanya kazi kwa kuzingatia umbali?

Kubadilisha ufanyaji kazi kutoka kwenye kituo cha redio na kwenda kufanyia nyumbani au mazingira mengine ya kazini inaweza kuwa ngumu, hasa ikizingatiwa kwamba ushauri mwingi unaopatikana mtandaoni hauwezi kushughulikia changamoto za kipekee zinazowakabili watangazaji wa Kiafrica wanaofanya kazi wakiwa mbali na vituo. Changamoto hizi zinaweza kujumuisha huduma isiyokuwa ya uhakika ya simu au huduma ya mtandao nje ya kituo, kutokuwepo kwa wafanyakazi kushughulikia maswala ya kiufundi, kukabiliana na mfadhaiko na afya ya akili, usumbufu kutoka kwa wanafamilia wakati wa kufanya kazi nyumbani, na kudumisha uaminifu wa hadhira licha ya mabadiliko ya programu ya kawaida na utangazaji. Kwa bahati nzuri, redio ni chombo kimojawapo cha habari chenye kurekebishika na watangazaji wanaweza kufanya marekebisho katika njia zao za kazi kuwasaidia kuzoea. BH2 hii inatoa habari ya kina juu ya njia za kuzoea utangazaji wa mbali, pamoja na kuweka bajeti na kuwekeza katika huduma za mtandao zenye kuaminika, kujiunganisha kwa ukaribu na wafanyakazi kushughulikia shida za kiufundi, kuwa makini na afya yako ya akili, na kutumia miundo ya redio zinazowafanya wasikilizaji wako washirikishwe, wahabarishwe, na kuburudishwa.

Nitafanyaje utangazaji wenye kuzingatia umbali kuwa wenye ufanisi?

  1. Kusanya vifaa na rasilimali utakazotumia kufanyia kazi ukiwa mbali na kituo cha redio
  2. Fanya mahojiano kwa kuzingatia umbali
  3. Kuondoa aina ya miundo au njia za kuzalisha vipindi vya redio
  4. Fanya jaribio na miundo salama ya redio
  5. Tumia tena mahojiano ya zamani na wataalam au rekodi kutoka kwenye vipindi vya zamani
  6. Punguza idadi ya wafanyakazi wanaofanya kazi kwa wakati mmoja
  7. Fanya mikutano kwa kuzingatia umbali/bila kukutana
  8. Tumia vyanzo na taarifa zilizorekodiwa
  9. Wekeza katika huduma nzuri za mtandao ili ufanye kazi kutoka nyumbani
  10. Tumia rasilimali za FRI kujenga au kuunda programu yako
Maelezo

 

1. Kusanya vifaa na rasilimali utakazotumia kufanyia kazi ukiwa mbali na kituo cha redio

Hapa kuna orodha ya vifaa kadhaa ambavyo unaweza kuvihitaji kufanyia kazi ukiwa mbali na kituo cha redio. Wakati wa taharuki ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19), hakikisha unasafisha vitu vyovyote unavyoleta nyumbani na uvisafishe mara kwa mara ukiwa nyumbani.

Hizi ndizo njia zingine ambazo uongozi unaweza kuzitumia kuhakikisha suala la kukaa umbali kati ya mtu na mtu wakiwa kazini na kuwasaidia wale wanaofanya kazi wakiwa mbali na kituo cha redio:

  • Chagua mfanyakazi fulani kutoa ushauri juu ya shida za uunganisho na kuwasaidia wale ambao hawajafahamu mambo ya kiufundi ya kufanya kazi kutoka nyumbani. Mfanyakazi huyu anaweza kusaidia wengine kushirikiana na watoa huduma.
  • Timu ya uzalishaji vipindi na utawala wanapaswa kufanya jitihada maalumu kuwafikia wasikilizaji kwa njia ya simu na kupitia njia nyingine yeyote inayowezekana kuona kama wasikilizaji bado wanasikiliza. Waombe watoe mrejesho na mapendekezo na wahimize waendelee kusikiliza kwa kipindi chote cha janga. Hakikisha unawafikia wasikilizaji wanawake. Wanawake wengine hawana redio au simu. Wahimize wasikilizaji wengine kuwasiliana na hawa wanawake, pamoja na wanawake walio katika familia, kuhakikisha kuwa wanahusiana na kituo na kuwasaidia kuwasiliana na kituo.
  • Uongozi unapaswa kutengeneza na kusambaza sera katika maeneo ambayo yameathiriwa na ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanajua hatua za usalama na vitendo bora vya kutoa habari wakati wa janga. Kwa mfano, wafanyakazi hawapaswi kufanya mahojiano na chanzo chochote kutoka kwa mtu binafsi isipokuwa kuna ulazima kabisa, na wanapaswa kuchukua tahadhari sahihi za kiafya na usalama kama vile kuvaa barakoa na glavu na kusimama angalau umbali wa mita moja kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kama wafanyakazi hawawezi kufanya kazi kutoka nyumbani, wanapaswa kuvaa barakoa wakati wote wakiwa ndani ya studio. Sera hizi zinaweza kusambazwa kupitia kundi la WhatsApp, mkutano wa mbali, na kubandikwa katika kuta ndani ya studio.

2. Fanya mahojiano kwa kuzingatia umbali

Epuka kukutana na kufanya mahojiano na watu isipokuwa tu kama kuna ulazima. Badala yake, fanya mahojiano kwa njia ya simu au mahojiano yaliyorekodiwa, na baada ya hapo hariri na kuhakikisha yanasikika vizuri. Simu nyingi hazina vinasa sauti kwa ndani kwahiyo, njia rahisi ya kurekodi mahojiano ya simu ni kuweka simu pembeni ya rekoda yako na kurekodi. Unaweza pia kutumia Skype kurekodi simu au mahojiano kwa njia ya video moja kwa moja kwenye programu. Punde tu baada ya mahojiano kuanza, bonyeza batani ya “Anza kurekodi”. Wakati utakaposubirisha simu, rekodi itaonekana katika sehemu ya kuchati kwa siku 30. Hakikisha unaipakuwa na kuihifadhi katika kipindi hicho ili usipoteze rekodi hiyo.

Image 1: Skype desktop

Image 2: Skype mobile

Chini hapa ni baadhi ya dondoo za kuzingatia wakati wa kufanya mahojiano kwa kuzingatia umbali. Unaweza kupendekeza kwa mtu unayemuhoji kufuata pia ushauri huu:

  • Zima sehemu ya kukupa taarifa katika simu yako (notifications) na muombe huyo mtu mwingine naye afanye hivyo. Hii itazuia mahojiano yenu kuingiliwa na simu nyingine zinazopigwa au taarifa zinazoingia katika simu zenu.
  • Angalia kiwango cha sauti kabla ya kurekodi. Unaweza kuhitajika kumuomba mtu unayemhoji kwenda sehemu iliyotulia. Hakikisha kuwa upo pia sehemu iliyotulia kwa kipindi cha mahojiano.
  • Usiwe unatembea au kuzunguka zunguka wakati wa mahojiano. Hii inaweza kuingiliana na huduma za mawasiliano au mapokeo ya sauti na inaweza kumfanya mhojiwa au wewe mwenyewe kutosikika vizuri.
  • Usisogeze simu yako au kompyuta wakati wa kurekodi – hii inaweza kusababisha mkwamo usiohitajika au kelele.
  • Usifanye kitu kingine chochote katika simu yako au kompyuta wakati unafanya mahojiano (mfano., kuangalia barua pepe, kutuma meseji).
  • Kama unafanya mahojiano ambayo yanarekodiwa na kurushwa baadae, muombe unayemhoji kutoa muhtasari wa mambo muhimu kabisa au taarifa mwishoni mwa mahojiano. Hii itakupa bite nzuri, fupi ya sauti ya kutumia katika programu. Epuka kufanya hivi wakati unarekodi mubashara kwasababu inaweza kumhamasisha anayehojiwa kuongea kwa muda mrefu, kitu ambacho kinaweza kuchelewesha kipengele kinachofuata.
  • Jiandae, weka umakini, na usikilize kwa uangalifu. Inaweza kuwa changamoto kufanya mahojiano bila kumuona mtu husika unayemuhoji. Ruhusu kuweka pumnziko kidogo na ukimya kadhaa, lakini hakikisha umejiandaa na maswali yako yote yanayofuata. Lakini epuka ukimya wa muda mrefu. Anayehojiwa anaweza kufikiri kwamba umeshakata simu, au ichukulie kama ishara ya kuendelea kuongea, zote hizi zinaweza kutatiza mahojiano.

Kama ilivyo kwa mahojiano yoyote, iwe ya mbali au ya uso kwa uso, ni muhimu kuandaa orodha ya maswali ili kukuongoza. Usiogope kumuuliza unayemhoji kufafanua au kuelezea zaidi mawazo yoyote yanayochanganya au mada, au jibu/mrejesho wowote ambao haueleweki. Ikiwa umechanganyikiwa kutokana na majibu/mrejesho unaoupata, wasikilizaji wako labda watakuwa pia wamechanganyikiwa! Ni muhimu kujihusisha na mhojiwa kwa heshima kwa kuuliza maswali mazuri na ya utafiti na kusikiliza majibu yake kwa umakini, pamoja na maswali ambayo hushughulikia maswala yanayohusiana na usawa wa kijinsia (Kwa mfano, kuongezeka kwa kiwango cha unyanyasaji majumbani wakati wa janga la ugonjwa wa virusi vya corona, COVID-19, na hatari ya wanawake kuambukizwa kama wafanyikazi walio katika mstari wa mbele). Fanya mahojiano yajikite katika mada husika kwa kuuliza maswali ya undani zaidi na upana zaidi. Ikiwa ni lazima, hariri mahojiano kwa umakini na kuhakikisha uwakilishi mzuri, sahihi, na usawa wa yaliyosemwa. Hakikisha kuwa vyote vilivyotolewa vimeakisi mahsusi mahitaji tofauti ya wanawake na wanaume.

Kuhariri sauti inajumuisha kuchagua kipi cha kujumuisha na kipi cha kutokujumuisha kutegemea na mwelekeo wa habari na mahitaji ya habari ya wasikilizaji wako. Wakati wa kuhariri simu iliyorekodiwa, kama ilivyo katika mahojiano ya uso kwa uso, uhariri wa msingi hujumuisha kuondoa sauti kama “ums” na “ahs” au maelezo mengine yasiyo ya lazima ili kuhakikisha kuwa rekodi inakuwa vizuri na fupi. Lakini utahitajika usikilize tena mahojiano yote, kuamua juu ya mwelekeo kusaidia kukuongoza juu ya kipi cha kuacha na kipi cha kufuta, chagua muundo wa uzalishaji (mfano., sehemu fupi zilizounganishwa pamoja, mahojiano au simulizi moja ya sauti), na pangilia mtiririko wa rekodi ya sauti ili kuleta mantiki. Hatua hizi zitakusaidia kutengeneza maudhui ya redio kutokea nyumbani ambayo ni muhimu, yenye ufanisi na yenye kuburudisha.

Jifunze zaidi kwa kusoma namna ya kuongoza watangazaji wa FRI kupitia uhariri wa sauti na mbinu za majohiano.

3. Kuondoa aina ya miundo au njia za kuzalisha vipindi vya redio

Njia zingine za kuzalisha vipindi vya redio sio salama kuzitumia wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) kwasababu zinahitaji kukutana na watu uso kwa uso, ambayo huongeza nafasi ya kueneza maambukizo. Unaweza kutaka kuondoa nakala ndogo za kumbukumbu, vox pops na michezo ya umma wakati sera za kukaa mbali kati ya mtu na mtu bado zikiwa zipo.

4. Fanya jaribio na miundo salama ya redio

Jaribu kujumuisha miundo ya redio ambayo ni ya kuburudisha na yenye kuhabarisha bila kujiweka wewe mwenyewe na wengine kwenye hatari. Ifuatayo ni baadhi ya mifano:

1.a href="https://training.farmradio.fm/conducting-a-panel-discussion-with-the-conference-call-feature/" target="_blank" rel="noopener">Conference call panel discussionMkutano wa maja diliano kwa njia ya mtandao: Unaweza kuwakaribisha watu wengi washiriki katika jopo la majadiliano kwa kutumia sehemu ya simu yako ya mkononi au mezani yenye kuruhusu kufanya mkutano kupitia kwenye simu. Kulingana na teknolojia inayopatikana wakati unafanya kazi kwa kuzingatia umbali, unaweza kutumia programu kama Skype, Hangouts za Google, au Zoom ili kuitisha mkutano wako. Kabla ya kurusha hewani programu mubashara, jaribu kufanya jaribio na washiriki wote ili waweze kujitambulisha na kusema kidogo kuhusu historia yao, kwani wanaweza wakawa hawajawahi kukutana wao binafsi. Hakikisha kuna usawa kati ya wanaume na wanawake katika jopo lako na zingatia kumjumuisha mtaalamu wa mambo ya usawa wa kijinsia.

2. Tape talk: Huu muundo wa usimuliaji habari ni mazungumzo kati ya mwenyeji (mtangazaji) na mwandishi ambaye ni sehemu ya mahojiano ya moja kwa moja na sehemu iliyorekodiwa sauti. Mtangazaji anamhoji mwandishi wa habari na, kama sehemu ya mrejesho wake kwa maswali ya mtangazaji, mwandishi wa habari anatumia sehemu za sauti kusimulia habari. Mazungumzo yaliyorekodiwa kwenye mkanda yanaweza kuzalishwa haraka, urefu wa mazungumzo unaweza kubadilika, na kuifanya kuwa ya kuelezea zaidi, na hutoa sauti ya “moja kwa moja” ya mwandishi kutoka kwenye eneo ambalo habari imechukuliwa, hata wakati ambapo mahojiano yamerekodiwa mapema.

3. Phone-in quizMaswali ya chemsha bongo: Maswali ya chemsha bongo kwenye redio yanaweza kufurahisha sana na kuhimiza ushiriki wa wasikilizaji. Njia rahisi na yenye ufanisi ya kuuliza maswali ya chemsha bongo ni kuuliza maswali ambayo jibu lake ni kusema kweli au sio kweli au kuuliza maswali yenye majibu ya kuchagua- au mchanganyiko wa maswali yote. Mhojiwa ambaye hutoa majibu sahihi zaidi ndiye mshindi. Kuna njia tofauti za kuuliza maswali ya chemsha bongo. Njia mojawapo ni kuuliza swali hilo hilo kwa washiriki wote, ambao lazima wajibu haraka iwezekanavyo. Njia nyingine ni kumuuliza kila mshiriki swali la tofauti na kuwapa kiasi cha muda wa kujibu. Walakini unaendesha jaribio, mshindi anaweza kupokea tuzo ndogo kutoka kwenye kituo cha redio, au kumtangaza hewani mshindi wa chemsha bongo na cheo chake. Ili kudumisha suala la kukaa mbali kati ya mtu na mtu, unaweza kuamua kuwapigia washiriki waliochaguliwa kabla au wasikilizaji wapige simu ili kujibu maswali. Hakikisha unatumia mbinu maalumu kuhimiza ushiriki wa wanawake, kwa mfano, kwa kuandaa namba ya simu kwa ajili ya wanawake tu, kushirikisha habari zaidi juu ya jinsi ya kushiriki, na kutangaza hamu yako ya kusikia maoni / majibu ya wanawake na vile vile ya wanaume.

4. Sauti zilizorekodiwa kwa njia ya WhatsApp: Badala ya kurekodi sauti za vox kibinafsi, waombe wasikilizaji warekodi maoni yao kwa kutumia huduma ya rekodi ya sauti kwenye WhatsApp. Ili kufanya hivyo, bonyeza tu na ushike ikoni ya kipaza sauti kulia mwa kibodi kwenye sehemu ya kuchati ya WhatsApp, rekodi sauti yako, toa kidole chako, na gonga mshale ili kutuma rekodi yako kwenda kwenye laini ya simu iliyoteuliwa. Mtangazaji anayepokea sauti iliyorekodiwa, anaweza kuipakua na kuihifadhi, kuhariri ikiwa ni lazima, halafu kuirusha hewani kwenye redio.

5. Michezo ya kuigiza: Inawezekana kuzalisha michezo ya kuigiza ya redio na wakati huo huo kudumisha miongozo ya usalama ya kukaa mbali kati ya mtu na mtu. Hakikisha kuwa kila muigizaji ana microfoni yake mwenyewe na amesimama angalau mita moja kutoka alipo muigizaji mwingine. Waigizaji wanapaswa pia kuvaa glavu na barakoa kama inawezekana. Jaribu kuwaweka kwenye chumba kikubwa (mfano., darasa lisilo na kitu au ukumbi wa jamii) au nafasi ya nje – hiyo pia itakusaidia kupata sauti ya kawaida, ya asili kwa baadhi ya matukio. Vizuizi hivi vinaweza kukuhitaji utoe igizo fupi, rahisi, lakini pia inaweza kusaidia wasikilizaji kuwasilisha miundo mbalimbali hewani kushirikisha habari muhimu juu ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).

Kwa orodha kamili ya miundo, soma Mwongozo kwa Waandishi kwenye miundo ya redio ya FRI.

5. Tumia tena mahojiano ya zamani na wataalam au rekodi kutoka kwenye vipindi vya zamani

Inaweza kuwa ngumu kufanya rekodi mpya kutokea nyumbani au kutokea studio, kwa hivyo inafaa kupitia rekodi za zamani na mahojiano ili kutumia tena baadhi ya rekodi hizo. Wasiliana na wataalamu wa kuaminika kwa njia ya simu kwa mahojiano yaliyohuishwa, lakini epuka kukutana uso kwa uso na wahojiwa wapya. Unapotumia tena rekodi ya zamani au unaporejea mahojiano ya zamani, hakikisha unawaeleza wasikilizaji kwamba mahojiano sio mapya na jaribu kuwasiliana pia na wahojiwa hao ili kutoa au kuona kama kuna jipya kuhusiana na mada. Waulize kama maoni yao yamebadilika au kama kuna mtaalamu mpya katika mada hiyo ambaye unapaswa kuzungumza naye. Kama taarifa hazijabadilika, ulizia kama kuna kitu kingine chochote kuhusiana na mada ambacho kitakuwa muhimu kwa wasikilizaji kufahamu. Mara tu utakapokusanya taarifa hizi mpya, zitaje tena mwishoni mwa mahojiano na wakumbushe wasikilizaji kwa mara ya pili tena kwamba mahojiano yalirekodiwa siku za nyuma.

6. Punguza idadi ya wafanyakazi wanaofanya kazi kwa wakati mmoja

Ongea na uongozi kuhusu utekelezaji wa sera ya kukaa mbali kati ya mtu na mtu. Hii inaweza kumaanisha kuwa na mtu mmoja tu kwenye sehemu ya kurekodia kwa wakati mmoja na mpokeaji mmoja kwenye meza au dawati la mapokezi. Kituo cha redio hakipaswi kuwa wazi kwa umma na wasikilizaji wanapaswa kuhimizwa kupiga simu kwenye kituo badala ya kutembelea kituo. Watangazaji wanapaswa kuhimizwa kufanyia kazi nyumbani pale inapowezekana. Wale ambao hawawezi kufanya kazi kutokea nyumbani wanapaswa kujaribu kufanya kazi kwa njia ya kubadilishana muda ili kupunguza kukutana na wafanyikazi wengine.

Ni muhimu kwa wale walio katika kituo kuvaa barakoa muda wote na kusafisha mara kwa mara nyuso za vitu kama vile meza, kompyuta, simu na microfoni na kitakatishi chenye pombe/kileo zaidi ya 60% ya ethanol au 70% isopropanol. Waongoza vipindi na mafundi mitambo wanapaswa kusafisha kabisa vifaa vyote na nyuso za vitu ndani ya studio kabla na baada ya muda wa hewani wa kipindi chao ili kuhakikisha usalama wao na usalama wa watu wengine.

Kuheshimu hatua stahiki za kukaa umbali kati ya mtu na mtu na kufanya kazi kwa kuzingatia umbali kunaweza kuwa na faida kubwa kwa afya ya akili za watu. Kama mtangazaji wa redio, ni muhimu kuzingatia afya yako ya akili pamoja pia na afya yako ya mwili na kujilinda ili kuhakikisha kwamba unaweza kuendelea kufanya kazi yako kwa ufanisi. Hapa kuna mikakati kadhaa:

  • Chukua mapumziko ya mara kwa mara na uzingatie kiwango chako cha nguvu uliyonayo na uchovu. Mwisho wa siku ya kazi, jaribu kupumzika ili kuzuia uchovu.
  • Uongozi wa kituo unapaswa kuwaangalia mara kwa mara wafanyakazi na kutoa miongozo na msaada pale inapobidi. Msaada unaweza kuwa kitu rahisi kama kupiga simu kusalimia, kutia moyo, kusikiliza changamoto na wasiwasi na kusifu kazi nzuriWatangazaji wanapaswa kuwataarifu wasimamizi wao kama watahisi kutokuwa salama katika kufanya kazi fulani.
  • Pale unaporipoti kuhusu COVID – 19, boresha afya yako ya akili na punguza kiwango chako cha mfadhaiko kwa kuweka vitu unavyovifahamu, ulivyo huru navyo karibu na wewe kukukumbusha maisha ya “kawaida”, kama picha ya familia yako na marafiki.
  • Fanya mazoezi mara kwa mara, kula vyakula vya afya, pata muda wa kutosha kulala na kunywa maji ya kutosha.
  • Jaribu kudumisha utaratibu wa kawaida iwezekanavyo.

7. Fanya mikutano kwa kuzingatia umbali/bila kukutana

Kama unafanya kazi kama sehemu ya timu, mtapaswa kufanya uzalishaji wa vipindi na aina nyingine ya mikutano kwa kuzingatia umbali kabla ya kurusha hewani kipindi. Tafuta programu ya bure yakuweza kuonana na kufanya mkutano (WhatsApp, Zoom, Skype, Hangouts za Google, nk.) na tumia sehemu ya sauti tu ili kupunguza matumizi ya bando na gharama. Weka ajenda ya mkutano wazi na watumie washiriki wote kopi kwa njia ya barua pepe kabla ya mkutano. Tazama mfano hapa chini:
Production meeting agenda

Amueni kama timu, ni mara ngapi mnahitaji kufanya mikutano ili kuhakikisha uzalishaji wa vipindi unaendelea vizuri pamoja na utendaji wa jumla wa kituo. Zingatia majukumu binafsi ya kifamilia yanayowakabili wahusika, kwa mfano, wale ambao wanahitaji kutunza watoto wachanga au wanafamilia ambao ni wagonjwa.

Kumbuka: Ni muhimu kutengeneza karatasi za kuonyesha mtiririko wa kazi za kutumwa kwa washiriki wote wa timu ya uzalishaji wa vipindi kabla ya programu kwasababu inawawezesha watangazaji, wazalishaji wa vipindi, mafundi mitambo na mwingine yeyote anayehusika katika programu kuratibu kazi zao ndani ya ratiba shirikishi. Pia ni kifaa muhimu cha kuweka vipengele vyako vya kazi katika mpangilio na kwa wakati. Kwa taarifa zaidi juu ya mada hii, soma Mwongozo kwa Waandishi ya fri juu ya kuandaa karatasi ya mtiririko wa kazi.

8. Tumia vyanzo na taarifa zilizorekodiwa

Katika hali ya kawaida, watangazaji wengi wa redio, hawataweza kuwashirikisha wengine rekodi zao kwasababu, isipokuwa kama ilivyoainishwa, vituo vinatangaza tu ripoti za asili. Kama mwandishi wa habari za redio, ni kinyume na miiko ya uandishi wa habari na ni potofu kutengeneza programu au sehemu ya habari ambayo inategemea mahojiano yaliyorekodiwa au sauti ambazo wewe au timu yako hamkurekodi bila kuwajulisha wasikilizaji wako. Jukumu la mwandishi wa habari ni kutoa ushahidi na kwa hivyo wanapaswa kujitahidi kutoa na kuripoti habari halisi wakati wowote inapowezekana.

Walakini, kwa programu ya dharura, ni muhimu kwamba hadhira yako inapata habari inayohitaji kwa njia zote muhimu. Hii inaweza kumaanisha kushirikiana na watangazaji wengine wa redio katika kituo chako au kutoka katika kituo kingine ili kushirikishana kwa njia ya kidigitali vyanzo vya habari, tafiti, rekodi au hata kuzalisha kwa pamoja programu kuhusu hali ilivyo katika eneo lenu. Kwamfano, mnaweza kushirikishana taarifa kutoka au kuhusu afisa wa afya katika eneo lenu ambaye ameweka kituo kwa ajili ya upimaji au anayesambaza barakoa. Labda mnaweza kushirikishana wimbo kutoka kwa mwanamuziki wa ndani kuhusu kujikinga na ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19). Mnaweza hata kushirikishana hii BH2 ikiwa umeona ni muhimu! Ikiwa tu utakiri chanzo cha habari hiyo, ni muhimu na inafaa kuishirikisha.

Unaweza kutaka kushauriana na watangazaji wengine katika eneo lako, mkoa, au nchi kupitia vikundi vilivyopo. Kundi la WhatsApp la FRI katika nchi yako ni jukwaa zuri kwa watangazaji wa redio kujifunza na kushirikishana mambo mbalimbali. Wasiliana na mwakilishi katika nchi wa FRI ili kuunganishwa katika kundi, au tuma barua pepe kwenda radio@farmradio.org na taja jina lako, nchi na kituo cha redio.

9. Wekeza katika huduma nzuri za mtandao ili ufanye kazi kutoka nyumbani

Kwa kufungwa kwa biashara zisizo muhimu ulimwenguni kote, inaweza kuwa ngumu zaidi kununua vifurushi vya data kwa simu yako ya mkononi au kompyuta. Kama inawezekana, wekeza katika huduma ya mtandao wa kuaminika ili uweze kufanya kazi kutoka nyumbani kwa siku kadhaa au wiki kwa wakati mmoja. Usitumie pesa yoyote isipokuwa unayo ruhusa au idhini ya awali kutoka kwa uongozi ili uweze kurudishiwa pesa. Ikiwa haiwezekani kwa kituo chako kufadhili gharama za mtandao wakati unafanya kazi kwa mbali, uongozi wa kituo unapaswa kuunda ratiba ambayo inaweka waandishi wa habari kwenye kituo kwa kubadilishana muda ambayo huwezesha wafanyakazi kukaa umbali wa mita kadhaa wawapo kituoni. Angalia sehemu #6 na #7 hapo juu.

Tazama mfano hapa chini wa bajeti ya muda wa maongezi ya simu ambayo mtangazaji wa Ghana angeweza kuwasilisha kwa uongozi wa kituo.

budget table

10. Tumia rasilimali za FRI kujenga au kuunda programu yako

FRI ina mkusanyiko mkubwa wa rasilimali za redio mtandaoni, pamoja na mahojiano na maandishi ya maigizo, mada za kilimo na mada zingine (pamoja na rasilimali zinazohusiana na masuala ya kijinsia). Namna-ya kuongoza watangazaji, simulizi za wakulima na mengi zaidi kukusaidia kuweka pamoja programu yenye kiwango cha hali ya juu kila wiki. Unaweza kuvinjari zana na rasilimali zetu kwa kutembelea, https://farmradio.org/radio-resources/

Wapi tena naweza kujifunza kuhusu njia za kukaa mbali?

Shirika la Redio la Watoto. COVID-19: Kuripoti tokea mbali & Zana za Utangazaji. April 2020. https://childrensradiofoundation.org/covid-19-remote-reporting-broadcast-toolkit/

Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari. CPJ Ushauri wa Kiusalama: Ikihusisha kuzuka kwa virusi vya Corona. 6 April 2020. https://cpj.org/2020/02/cpj-safety-advisory-covering-the-coronavirus-outbr.php

Mtandao wa Uandishi wa Habari Duniani. Webinar: Kubaki salama wakati unaripoti juu ya COVID-19. 15 April 2020. https://www.youtube.com/watch?v=KEcBYPGh8b0&feature=youtu.be

Wangui, Irene. Rasilimali kwa Wanahabari wa Kiafrika zinazohusu janga hili. Mtandao wa Uandishi wa Habari Duniani. 9 April 2020. https://ijnet.org/en/story/resources-african-journalists-covering-pandemic

Acknowledgements

Imechangiwa na: Maxine Betteridge-Moes, mwanahabari huru na mshauri wa zamani wa rasilimali Utangazaji wa FRI Ghana.

Rasilimali hii imeandaliwa kwa msaada wa kifedha wa Serikali ya Canada iliyotolewa kupitia Global Affairs Canada