Jinsi ya kuwafikia wanawake wakulima vizuri

Je, mpaka wakati huu sinimekuwa nikiwahudumia wakulima kina baba na kina mama vizuri?

Kwa miaka mingi, vipindi vya redio vimekuwa vikiwahudumia wakulima wanaume. Watangazaji wanaume wakiwahoji wataalamu wanaume juu ya mazao na mifuko wanayozalisha wanaume.

Leo hii tinajua kuwa wanawake wanafanya kazi shambani-sawa na wakulima wanaume.
Pia wanalisha familia na kuwahudumia watoto wadogo na kuwalea wazee

Hivyo wanawake ni watu muhimu katika kukua na kuendelea kwa familia. Kwahivyo ni muhimu kwa vipindi vya kilimo –kuwahudumia wakulima wa jinsi zote wanawake pamoja na wanaume.

Fikiria hili. Je, ni kweli unawahudumia wakulima wako wanawake? Tazama dondoo zifuatazo kuona jinsi gani umekuwa ukifanya, Na weka katika matendo dondoo zote uwezavyo!

Muongozo huu utanisaidiaje kuwahudumia wasikilizajii wangu vizuri?

  • Wakulima wanawake watapata taarifa wanazo hitaji ili kuweza kulima vyema.
  • Wanawake wakulima wataweza kutoa maoni yao juu ya masuala yenye manufaa kwao.
  • Wanawake wakulima watafurahia vipindi vyako zaidi.
  • Wakulima waanaume watajifunza Zaidi vitu ambavyo ni vya muhimu kwa wanawake wakulima na watavitilia maanani.

Muongozo huu utaniwezeshaji mimi kuzalisha na kurusha kipindi kizuri?

  • Inanipatia dondoo ambazo ninaweza kuzifanyia kazi na kuniwezesha kuwavutia wakulima wanawake –wasikilizaji na kuongeza wasikilizaji.
  • Inanipa muongozo wa namna ambayo nitaweza kuangalia masuala ya kijinsia katika kituo cha redio.

Ninaazaje?

  1. 1) Wapatie wakulima heshima wanayostahili.
  2. Tafuta kitu gani ni cha muhimu kwa wakulima wanawake na kijumuishe katika kipindi.
  3. Tangaza muda ambao wakulima wanawake wanaweza kusikiliza kipindi.
  4. Washawishi wakulima kina mama kuongea redioni.
  5. Hakikisha kituo chako –kina tambua masuala ya kijinsia.

Maelezo ya kina

1. Wape wanawake wakulima heshima wanayo stahili

Kama ilivyotajwa hapo juu, wanawake wanafanya kazi nyingi katika-shuguli za kilimo. Na wanafanya kazi hizi wakiwa wanawalea watoto, wanahudumia familia zao na kuwalea watu wazima. Kazi zao ni za muhimu katika ukuaji wa familia. Katika kila kitu unachokifanya—kuandaa kipindi, kufanya mahojiono, kutangaza,—hakikisha unakumbuka kuonyesha umuhimu wa wakulima wanawake kwa kutaja kzai zao ngumu wanazo fanya, fanya maamuzi ya muhimu kwa usalama na afya za familia zao, na siku zote wanzuiwa na mawazo hasi na sharia za kijinsia zinazo wabana. Mwisho kumbuka, kuonyesha, jinsi utofauti katika uchumi-jamii ambayo wote wanawake na wanaume wanachangia katika jamii na majumbani mwao.

Kwa mfano:

  • Waongelee wanawake kama wakulima, sio kama wake wa wakulima.
  • Ongea nao kwa kutaja majina — wao ni watu.
  • Waulize maoni yao juu ya mambo muhimu ya kilimo. Watakushangaza kwa jinsi wanavyojua mambo kwa undani.
  • Onyesha simulizi za mafanikio ambazo zinaonyesha utofauti wa majukumu kijinsi, kwa mfano, wanawake kujihusisha na uzalishaji wa mazao biashara au wanaume kujumuika katika kufanya maamuzi ya afya ya familia.

2. Tafuta kitu gani ni muhimu kwa wanawake, na kiongelee

Kwa kawaida tunajua kuwa kazi za shamba ni kazi ngumu na huwa ni kazi zinazo fnywa na wanaume. Na huyu mwanamke kazi zake ni kutunza bustani za mboga. Lakini wanawake wanashughulika na shughuli zote za kifamilia zinazo changia katika afya za familia ikiwemo, ubora na kiasi cha mavuno. Kwa mfano:

  • jinisi ya kuboresha udongo
  • lini muda wa kuuza
  • jinsi ya kuboresha lishe za mazao
  • jinsi ya kuata mikopo nafuu kuboresha kilimo
  • jinsi ya kutunza fedha za familia

Nenda vijijini na fanya vikao na wanawake. Waulize ni vitu gani muhimu wanavyo vikabili katika shughuli za kilimo. Wakati wa mahojiano, taja baadhi ya mada hizo hapo juu ili wasiongelee tu “bustani” za nyumbani. Sikiliza vizuri na, mwishoni, waambie kitu ulichosikia kama kipao mbele chao. Kisha katika kituo cha redio fikiria namna ambayo utaweza kujumuisha mambo haya katika kipindi.

3. Tangaza kipindi muda ambao wakulima wanawake wataweza kusikiliza

Unaweza ukawa unazalisha kipindi chenye taarifa za manufaa kwa wanawake wakulima, lakini utakapo rusha kipindi, lakini kikiruka muda na siku ambao wakulima wanawake hawataweza kusikiliza, kazi yako itakuwa imepotea! Unapotembelea vijijini na kukutana na wanawake, wauliza ni muda gani wanaweza kusikiliza kipindi cha redio. Waulize wanaume swali hilohilo. Kama wanaume na wanawake wanaweza kusikiliza kipindi kwa muda mmoja basi rusha kipindi katika muda mmoja. Lakini kama wakulima wanawake watakuwa wanasikiliza muda tofauti na wanaume, basi utahitajika kurudia kipindi chako muda ambao wanawake watasikiliza, ili wakulima wote waweze kufikiwa na vipindi. Ingawa mfumo huu ni mgumu kidogo pale unapokuwa na -simu za wasikilizaji katika kipindi, ambapo kipindi kinalazimika kuwa hewani wakati huo. Kwa hali hiii, utahitajika kuongezea kipengele cha simu za wasikilizaji moja kwa moja pindi utakapo rudia kipindi-kilichorishwa awali. Au kwa namna nyingine, unaweza kuandaa vipindi viwili tofauti vya kilimo, kipindi kimoja kitawalenga wakina mama na kipindi kingine kitawalenga wakina baba wakulima.

4. Kuwahimiza wanawake kuongea/kuchangia katika kipindi

Katika tamaduni nyingi, wanawake wananyamaza na kuwaacha wanaume waongee— wenyewe, juu yao, juu ya wake zao na juu ya familia zao. Kakini muda unavyoenda mambo yanabadilika. Wanawake wanahaki ya kuongea juu ya mambo yanayowahusu. Na jamii yako itakuwa ina afya na salama na yenye nguvu kazi kama sauti ya wanawake itasikika na kuonekana kuwa ni sauti ya msingi katika kujadili vitu muhimu katika jamii. Angalia wapi wanawake wanaweza kuwa na uhuru wa kuongea, inaweza kuwa ni majumbani mwao, katika mashamba yao, au katika vikundi vya marafiki, na kuwatembelea huko. Katika muongozo huu utakutana na mambo muhimu yatakayo kuwezesha kuwashawishi wanawake kuzungumza katika kipindi. Mambo haya ni:

  • tafuta wanawake ambao wanaujasiri wakuzungumza redioni
  • wahiji wanawake katika vikundi
  • kuruhusu wanawake kuzungumza na kutoa maoni yake bila kujulikana

5. Fanya kituo chako cha redio kiwe kinazingatia-mambo ya kijinsia

Haya ni mambo ambayo msikilizaji anaweza kutambua kama kituo cha redio kinazingatia-jinsia au lah. Angalia vitu hivi:

  • Unawaalika wanawake kutembelea kituo cha redio muda wa mchana ambapo ni salama kwao kusafiri?
  • Una vyoo vyenye kukidhi mahitaji ya wanawake na wasichana?
  • Kila mtu katika kituo cha redio anawaheshimu wanawake kama wanaume wanavyoheshimiwa?
  • Wasikilizaji wanasikia sauti za wanawake katika- kipindi wakiendesha kipindi kama watangazaji wa kiume wanavyofanya? (Kwa ujumla kituo cha redio hakina mazoea ya kujumuisha sauti za wanawake katika kipindi.)
  • Je, kituo chako cha redio kinasera za usawa wa kijinsi ana zinafuatwa na sera hizi kupata ushirikiano katika ngazi zote za shirika?

Namna nyinginezo ambazo unaweza kumhudumia mkulima mwanamke vyema

Kutumia –line tofauti za simu kwaajili ya wanawak

Kwa kawaida wanawake wanaumiliki mdogo wa simu kulinganisha na wanaume. Kama asilima 0% ya wanaume ndio wamiliki wa simu basi asilimia 90% ya simu zitakazo pigwa zitakuwa ni za wanaume. Lakini, ukiwa na line mbili tofauti, moja kwaajili ya wanawake kupiga basi utakuwa na asilimia 50% wanawake watakao piga simu redioni! Ingawa kuna gharama zitakuwepo, na kusimamia kuhakikisha kuwa lini ya wanawake inatumiwa na wanawake tu, hii ni moja kati ya namna nzuri ya kuweza kuwafanya wanawake wahisi kuwa maoni yao yanasikika redioni na ni yadhamani.

Watembelee wakulima wanawake

Panga usafiri ili uweze kuwafikia wakulima vijijini. Himiza wanawake kutembelea redioni ili uweze kuwa na maudhurio mazuri. Kama wewe ni mtangazaji wa kiume, unapowatembelea wakulima wanawake nenda na mtagazaji wa kike pia. Hii itaweza kuwafanya wanawake kujisikia vizuri na wawe wazi kuzungumza.

Watafute wanawake wanya ujasiri wa kuongea redioni

Unapompata mwanamke mwenye ujasiri wa kuongea redioni na mwenye mchango muhimu na maoni ya kutoa, chukua namba zake za simu ili uweze kumuhoji kwa kina hapo baadae endapo utakuwa na maswali zaisi. Hii itawashawishi wanawake wengine kupata shauku ya kuzunguza katika kipindi.

Kuwahoji wanawake katika vikundi

Uki muhoji mwanamke mmoja peke yake, mwanamke anaweza akawa na hofu lakini utakapo wahoji wanawake katika vikundi kila kitu kinabadilika! Wanawake wanahisi kuwa na “nguvu katika kikundi”. Na mwanamke mmoja akitoa maoni mwanamke mwingine atahisi kuwa ataweza kuzungumzia jambo kwa undani Zaidi na kutoa maoni ya undani zaidi. Na mwanamke wa tatu atahisi kuwa anauwezo wa kuchangia mada iliyotajwa na kupeleka mazungumzo kwa undani zaidi.

Wapatie simu za mkononi wanawake wakulima wanaoshi vijijini ndani maeneo yasiyo sikika

Katika baadhi ya vijiji, kunawanawake wasio na uweza wa kupata huduma za simu, kama utaweza kununua, mpatie mwanamke mmoja utakatye muamini katika kijiji hicho ambaye ataweza kutumia simu hiyo kupiga simu redioni na kutoa maoni yaeke.

Jumuisha maisha na uzoefu wa wakulima wanawake katika kipindi

Wote tunapenda kusikia taarifa za watu wenye maisha kama yetu. Jinsi gani watu wengine wanakabiliana na changamoto tunazo zikabili? Nini kinawapa furaha na nini kinawahuzunisha? Wahoji wanawake wakulima na wape nafasi ya kusimulia maisha yao redioni. Hii itawapa matumaini wanawake wengine wenye matatizo kama hayo.

Fanya kazi na vikundi vya wanawake

Tafuta vikundi vya wanawake ambayo tayari vinafanya kazi na waalike wachangie katika kipindi na kusikiliza kipindi na kukusanya maoni yao ni jinsi gani kipindi cha kilimo kinawanufaisha wao kama wanawake wakulima. Kwa taarifa Zaidi kuhusu vikundi vya kusikiliza redio, bofy hapa (Kwa kingereza tu).

Tumia maeneno ya wakulima wanawake

Baadhi ya maeneo wanawake wana maneno wanatotumia kuelezea aina ya mazao na mbinu za kilimo. Haya maneno siku zote hayajulikani na watangazaji wa kiume—au hata wakulima wa kium! Tumia maneo ambayo wanawake wanayajua na wanayaelewa.

Mruhu mwanamke kuchangia mawazo yake pasipo kujulikana majina yake kwa mada nyeti

Kama mwanakme amefanyiwa kitu kibaya katika mazingira yake ya kazi, au nyumbani kwake, lakini anaogopa mambo mabaya yatamkuta endapo atachangia maoni yake, msaidie kufikisha simulizi ya maisha yake kwa wasikilizaji. Ikiwa unajua jina la mwanamke na umamuamini, uhitaji kutangaza jina lake au taarifa yoyote. Unaweza pia kubadilsha sauti yake kwenye kompyuta au unaweza kurusha smulizi lake pasipo kutaja majina yaje kabisa. Utaona kuwa kwa kurusha simulizi lake utawasaidia wakulima wanawake wengine wenye hali kama yake kuweza kupaza sauti zao. Hii itawasaidia na pia itakusaidia wewe kama mtangazaji, kuweza kurusha mambo ya undani zaidi. Kumbuka mbali na kuficha jina la mhojiwa, na kubadilisha sauti yake, pia ni muhimu kutotaja taarifa zinginezo ambazo zinaweza kumtambulisha katika simulizi.

Wakulima wanawake ni wataalu pia!

Baathi ya wakulima wanawake wanajua vyema namna ya kufanya kilimo bora kama wanavyojua wataalamu wa kilimo. Wahoji wakulima hawa. Taarifa zao zitakuwa za dhamani kwa wakulima wengine, na mifano yao itasimama kuonyesha kuwa wanawake wanadhamani.

Badilisha jinsi unavyo wahoji wakulima wanaume na wataalamu wanaume

Kama mtaalamu anasema kuwa chanjo ya ngombe itawanufaisha wakulima (wanaume), uliza jinsi gani chanjo itawanufaisha wakulima wanawake na familia zao. Na hakikisha unauliza kuwa kama huduma za chanjo zinapatikana kwa wanawake kama wanavyo pata wanaume.

Usiongee na wanawake tu juu ya bustani zao za mboga

Ni kweli kwamba wanawake wengi wanafanyakazi nyingi za jikoni na za bustani. Lakini wanapenda kufanya shughuli za shambani za familia pia. Na wanakuwa na ushauri mzuri lini unaweza kuuza mazao au mifugo, au namna nzuri unayoweza kutunza udongo,au je, ni vyema kukopa au kotokopa hela kununua pembejeo za kilimo.

Wafundishe wanawake jinsi ya kutumia simu za mkononi

Baadhi ya wanawake hawakupata nafasi ya kujifunza kuandika shuleni. Hata wakiwa na namba za simu wanaweza wasijue jinsi ya kutumia. Tengeneza namna ambayo itawasaidia kukumbuka namba gani wanaweza kubonyeza, Jaribu mfumo huo na wanawake mmoja mmoja kama inafanyakazi, kama inafaa, tangaza mfumo huo mara kwa mara redioni.

Huu ni mfano wa namna ya kumbukumbu unayoweza kutafsiri na kuweka katika nyimbo. Unaweza ukawa na mfumo mzuri Zaidi. Labda simu yako ya mkononi inaweza ikawa na namna ya kutunza kumbukumbu, ambayo unaweza kutumia kukumbuka namba za kubonyeza pindii unapohitaji kutumia simu. Cheza sauti hii muda wa mapumziko kila wiki. Waulize wanawake kama mfumo huu umewwza kuwasaidia kutumia simu zao za mkononi.

Kupitia simu yako ya mkononi
Unaweza kuongea na ulimwengu
Unahitaji tu kujua
Ni namba gani ya kubonyeza
Hizi hapa, kutoka kushoto kwenda kulia:
– mstari wa juu: moja mbili tatu,
– mstari unaofuatia: nne tano sita,
– mstari wa tatu: saba nane tisa,
– msatari wa mwisho: nyota sifuri reli

Kuwa na furaha unapotangaza!

Kumbuka kuwa vipindi vinayo furahisha na vinavyo elimisha vinamanufaa kwa wasikilizaji wako. Tafuta namna ya kujumuisha simulizi za kale na za kisasa na nyimbo katika vipindi vyako;hii itawavutia wote wanaume na wanawake katika kipindi.

Furahia mafanikio

Kila siku wanawake wakulima wanakabiliana na changamoto na kufikia malengo mazuri katika kazi zao za kilimo. Tafuta simulizi zenye kuonyesha mafaniio haya na rusha redioni.

Wapi pengine ninaweza kujifunza Zaidi jinsi ya kuwahudumia wakulima wanawake redioni?

Adamou Mahamane, Fatouma Déla Sidi, and Alice Van der Elstraeten. 2014. Guidelines for the production of gender responsive radio broadcasts . Food and Agriculture Organization of the United Nations. http://www.fao.org/3/a-aq230e.pdf

Maana

Jinsia: Usawa wa kijinsi ni neon linalo maanisha wanaume na wanawake kupata haki sawa, wakati huo huo ukiheshimu utofauti wao. Inahitaji jitihada kuleta usawa wa kijinsi kutokana na utofauti mkubwa uliopo kwa sasa ambao unawaweka wanawake na wanaume katika hali mbaya—kwa mfano: kutumia simu tofauti kuhakikisha kuwa redio inapaza sauti nyingi za wanawake kama zinavyopaza sauti za wanaume, au kubadilisha muda wa mikutano au mafunzo ili wote wanawake na wanaume waweze kuhudhuria.

Usawa wa kijinsi: Usawa wa kijinsi inamaanisha wote wanawake na wanaume, kufurahia haki, fursa, na nafai za kimaisha hazizuiwi au kutengwa kutokana na jinsia. Usawa wa jinsia unahakikisha kuwa mtazamo, shauku, mahitaji, na kipaombele cha mwanaume na wanawake vinapewa uzito sawa nan a vinatazamwa katika majukumu na hatua za-kufanya maamuzi—katika mazingira ya kazi. Kwa mfano: wanawake na wanaume wana haki sawa za fursa za kazi/ajira, mafunzo, promosheni, mazingira ya kazi, na mishahara. Uswa wa kijinsia inachangiwa na inajumuisha mifumo mingine ya kijamii kama kiwango cha maendeleo, umri, kabila, au mwelekeo wa kijinsia, na jitihada kupata usawa katika maeneo haya.

Hatua juu ya masuala-jinsi: Hatua juu ya masuala ya kijinsia ni kitendo cha kuchukua maamuzi kusahihisha ubaguzi wa kijinsia au upendeleo wa kijinsi ili kuhakikisha usawa wa kijinsi. Inamaana kuwa vipindi vitaandaliwa kwa kuzingatia usawa wa kijinsia, kwamba mahitaji ya wanawake na mahitaji ya wanaume yatazingatiwa, ubaguzi hauta hautakubalika, na usawa wa kijinsi utahimizwa.

Shukrani

Imechangiwa na: Doug Ward, na kuongezewa na Caroline Montpetit, Sylvie Harrison, na Vijay Cuddeford

Mradi umefadhiliwa na serikali ya Cnada kupitia kitengo cha mahusiano ya kimataifa

The translation of this resource was made possible with the support of USAID’s New Alliance ICT Extension Challenge Fund, through the International Fund for Agricultural Development in Tanzania. For more information about the Fund, please see: https://www.ifad.org/