Kuhoji wataalamu: Operesheni bora Zaidi kwa watangazaji na wataalamu

Utangulizi

Kuhoji wataalamu hufaidi Zaidi vipindi vya wakulima kwenye redio. Hupatia wakulima ujumbe wa kutegemewa kutoka kwa vyanzo madhubuti. Usisahau kuwa baadhi ya wakulima ni wataalamu pia.

Ni muhimu kufahamu kuwa mwongozo huu wa utangazaji unaweza kutumiwa na watangazaji pamoja na wakulima kwa sababu ni muhimu kwa makundi yote mawili kujua majukumu yao halisi tabia ya wengine wanaohusishwa kwenye mahojiano haya.

Mahojiano mwafaka kutoka kwa wataalamu yanawezaje kusaindia kuhudumia wasikilizaji kwa njia bora zaidi?

  • Hakikisha kuwa wasikilizaji wanapata maarifa yenye umuhimu na yaliyosasihwa kila wakati.
  • Hujenga maarifa ya wasikilizaji na uzoefu kutokana na ufafanuzi, ujuzi au kutokana na hekima ya kale.
  • Hupatia wakulima ujasiri kuwa wanatumia njia mwafaka za ukulima.
  • Husaindia wakulima kupata maarifa na kuelewa njia mpya za ukulima.
  • Husaindia wasikilizaji kuzungumza na maafisa wenye utaalamu kwenye sekta ya ukulima katika jamii zao.

Mahojiano bora husaindiaje kuibuka na vipindi bora vya redio?

  • Huboresha utendakazi wema kati ya kundi la wanaredio na wataalamu kwenye sekta ya ukulima.
  • Huhakikisha kuwa wataalamu wa ukulima wanachangia pakubwa kwenye vipindi vya redio.

Je, nitaanza vipi kufanya mahojiano?

  1. Uwe umejitayarisha kabla ya kuanza mahojiano
  2. Ujue kufanya utangulizi na kutamatisha mahojiano
  3. Uwe na heshima
  4. Tumia ujuzi mzuri wa kufanya mahojiano yako
  5. Fahamu iwapo kuna tofauti kati ya kuhoji wataalamu na wakulima wa kawaida
  6. Unafaa kuelewa nyanja zenye mvuto Zaidi, zile zenye mitazamo mbali mbali na ujuzi kwa jumla
  7. Unafaa kuwa na uwezo wa kutatua shida
  8. Uwe na uwezo wa kukabili tamaduni na vizuizi vyengine vya mahojiano. Uwe pia na ujuzi wa kufanya mahojiano
  9. Wanaofanya mahojiano na wanaofanyiwa wanafaa kuwa watu wa jinsia moja. Kwa mfano, wanaume wahoji wanaume na wanawake wahoji wanawake
  10. Uwe na uwezo wa kutengeneza uhusiano mzuri

Maelezo Zaidi

1. Uwe umejihadaa

Kwa mwenye anahoji:

  • Chagua swala muhimu la kujadili na upeo wa mahojiano. Kwa mfano;
    - “Leo tutajadili kuhusu kulisha kuku wadudu. Tutaangazi aina mbali mbali ya wadudu wanaotumika, njia muhimu za kuwanasa na kuwafuga na faida na changamoto za wakulima”.
  • Unafaa kupanga mahojiano yako vizuri ili kuhakikisha kuwa wanaohojiwa watapatikana na hakikisha kuwa umewafahamisha mahojiano watachukua muda wa masaa au dakika ngapi.
  • Fanya utafiti kuhusu mada ili upate ufahamu kuhusu maswala na maswali ambayo unaenda kujadili. Kama unahoji wakala, jaribu kuhoji wakulima kwanza ili upate maswali ambayo wangetaka kujibiwa na mtaalamu.
  • Fanya utafiti kiasi kuhusu mtaalamu unayetaka kuhoji na ujue nyanja ambayo amebobea.
  • Tayarisha maswali yako kwa umakini ili yaweze kuongoza mtaalamu asiende nje ya mada. Usipofanya hivyo, mtaalamu anaweza kuenda nje ya swala kuu mnalojadili na azungumzie maswala mengine yasiyo na umuhimu.
  • Hakikisha umefahamisha unayemhoji kuwa mahojiano yatarekodiwa na yanaweza kupeperushwa na watangazaji.
  • Hakikisha mtaalamu anajua watakaosikiliza. Kwa mfano, wakulima wadogo wadogo wanaolima mihogo na wanaowezakuwa hawana elimu na hivyo kuwa na uwezekano wa kukosa kuelewa iwapo atatumia lugha ngumu. Je, mtangazaji anafaa kutumia mtaalamu orodha ya maswali yatakayojadiliwa? Hata kama wengi huonelea kuwa ni vyema mtangazi kutumia mtaalamu maswali, kuna adhari ya kufanya hivyo. Kwa mfano; Kupatia mtaalamu orodha ya maswali kuna hatari kwa sababu anaweza kudhibiti mahojiano na kuamua ni maswali gani ya kujibu na kuacha mengine. Hatari nyengine ni kuwa badala ya kujibu swali moja kwa muda kabla ya kujibu swali lengine (jambo ambalo husaindia wasikilizaji kupata maarifa kwa mpangilio), mtaalamu anaweza kujibu swali moja na kisha kutoa hotuba inayojibu maswali mengine kadha wa kadha bila kuyaangazia kwa undani n ahata anaweza kukosa kutoa nafasi ya wasikilizaji kufuatilia. Kwa sababu ya vizingiti hivi, inapendekezwa kuwa mtangazaji afahamishe mtaalamu kabla ya mahojiano (Kwa mfano wakati anapopanga siku na muda wa mahojiano kwa kupiga simu) kuhusu mada itakayojadiliwa na atoe orodha ya maswali machache ambayo wasikilizaji wanatarajia yajadiliwe bila kutoa maswali halisi yatakayompa mwongozo wa majadiliano.

Kwa Mtaalamu:

  • Pitia na ujifunze mada kuu itakayojadiliwa ili ujue maswali muhimu na upate ujasiri wa kutosha.
  • Zima simu yako kabla ya kuaza mazungumzo ya ana kwa ana ili kupunguza kusumbuliwa wakati wa mahojiano.
  • Ni muhimu kunakili maswala makuu ambayo utazungumzia ili kuepuka kukosa la kusema katikati ya mahojiano hata ingawa hauna maswali halisi ya kukuongoza kwenye mahojiano.Hata hivyo, sio vizuri majibu yako kusomwa kwenye redio yakiwa yameorodheswa kana kwamba ulikuwa unatoa hotuba. Mahojiano yanafaa kuwa mazungumzo, ukijibu maswali kama unavyoulizwa kwa njia ya mpangilio na inayoeleweka na wasikilizaji.
    - Kwa mfano, kwenye taifa la Uganda, mtaalamu anaweza kujiweka tayari kwa mahojiano kwa kuorodhesha vizingiti vya uzalishaji wa ndizi vinavyohusiana na jinsia: 1) Mwanamke aliyeolewa hafai kuvuna ndizi kwa sababu ataonekana kama mwizi; 2) Wanawake hawafai kuuza ndizi zinazozalisha vinywaji; 3) Wanawake hawamiliki mashamba ya ndizi.

Kumbuka: Ni wajibu wa mtangazaji kuchagua mada ya kujadiliwa na kudhibiti mahojiano kwa sababu ndiye anayejua lengo la vipindi vya redio na anafaa kuhakikisha kuwa wasikilizaji wanapata maarifa wanayofaa.

2. Utangulizi na kutamatisha

Kwa mwenye anahoji:

Utangulizi:

  • Kama uliwahi kuhoji mtaalamu hapo awali, mkumbushe kuhusu vipindi mlivyorekodi hapo mbeleni. Mueleze umuhimu wa vipindi hivyo vya awali na umpe nafasi apate maoni kutoka kwa wasikilizaji wakielezea jinsi walivyofaidika.
  • Kabla haujaanza mazungumzo na mtaalamu, mpe tabasamu na ufanye mandhari kuwa bora Zaidi ndipo umtambulishe kama inavyostahili.
  • Hakikisha umefanya utangulizi mzuri wa mahojiano wakati unaporekodi au kupeperusha mahojiano hewani. Kwa mfano, taja swala ambalo unataka kuzungumza na mtaalamu, uzoefu wa mtaalamu wa kujadili swala hilo na manufaa ya majadiliano hayo. Kisha tambulisha mtaalamu ukieleza jinsi alivyo na uwezo wa kujadili na kutatua swala hilo na ueleze kuwa unataka mtaalamu azungumzie swala hilo kwa undani. Kwa mfano;
    • “Mabadiliko ya hali ya anga yanaendelea kukumba wakulima kwa adhari kubwa haswa kwenye maeneo kame. Ni utaratibu upi wakulima wanafaa kuzingatia ili kukabiliana na hali hii? Studioni tunaye John Phiri, mtaalamu wa maswala ya mabadiliko ya hali ya anga na madhara yake kwa uzalishaji wa mimea. Bwana Phiri atatusaindia kujua njia za kukabiliana na swala hili.”

Kutamatisha:

  • Kumbusha wasikilizaji kuhusu lengo la mahojiano na utaje kwa kifupi baadhi ya maswala ambayo mtaalamu aliangazia. Kwa mfano:
    • "Kama mlivyosikia Patience Abdulai kutoka Tumu ametueleza uzoefu wake kuhusu kuhifadhi ukulima. Amesema kuwa faida tatu kuu anazopata kutokana na uhifadhi wa ukulima ni kuwa kwa sababu ni mja mzito na anataka mapumziko, kupalilia kiasi ni rahisi. Kupanda aina tofauti ya mbegu kila msimu imesaindia jamii yake kupanda vyakula wanavyotaka, na husaindia kwa soko na kupata vyakula vyenye lishe bora. Hatimaye baada ya kuhusika kwenye uhifadhi wa kilimo kwa miaka michache, ameanza kuelewa kuwa michanga yenye rotuba huleta mazao bora, na kuwa ijapokuwa itachukua miaka mingi, kuna tofauti zenye faida sasa”. USISEME TU; “Mmesikia kutoka kwa Patience Abdulai kutoka Tunu akitueleza kuhusu umuhimu wa kuhifadhi kilimo."
  • Unaweza pia kuomba mwenye umehoji kutaja hoja muhimu Zaidi alizozungumzia kwa ufupi.
  • Kumbuku kutoa shukrani kwa mtaalamu: Kwa mfano:
    • "Tunashukuru sana kwa kuzungumza nasi leo na tunatumaini kuwa utakuwa nasi kwenye vipindi vijavyo”. Ama kwa ufupi sema “Tunashukuru kwa kuwa kwenye kipinde chetu siku ya leo."
  • Hakikisha kuwa umehifashi kipindi ulichorekodi kwa kutumia jina la mwenye umehoji, tarehe na mada aliyozungumzia ili kusiwe na shaka utakapotaka kutumia siku za usoni.

3. Uwe na heshima

Kwa mwenye anafanya mahojiano na kwa mtaalamu;

  • Epuka kubadilisha tarehe ya mahojiano dakika ya mwisho. Fahamu kuwa mwenzako ako na majukumu mengine na umkumbushe mara kadhaa iwapo unataka kubadilisha siku ya mahojiano.
  • Epuka kukatiza mahojiano mara kwa mara.
  • Fika masaa mliyoagana bila kuchelewa.
  • Sikiza mwenzako kwa umakini.
  • Epuka kuonyesha kuwa uko na hasira, umechoka, umesongwa na mawazo au umeboeka kupitia kwenye uso au kutokana na vitendo vyako.
  • Epuka kupinga uzoefu wa mwenzako. Kwa mfano; “Wakulima hawana uwezo wa kupata mbegu. Ni wavivu sana na hawawezi kushughulika kuzipata”. Ama “Wataalamu hawasikizi wakulima kwa umakini na hivyo idara ya ukulima haitashughulikia swala hili.”
  • Epuka mabishano ambayo kila mmoja hujuhusi kuwa ako sahihi na hujaribu kuonyesha kuwa mwenzake amekosea na hajahitimu au analenga hoja husika.

Kwa mwenye anafanya mahojiano:

  • Maliza mahojiano wakati uliokuwa umepangiwa. Iwapo kuna maswala mengine unataka kujadili, uliza unayemhoji iwapo anaweza kukupa muda Zaidi. Kama hatakubali, agiza mfanye mazungumzo wakati mwingine.
  • Epuka kuuliza maswali ya kibinafsi au yale ambayo hayahusiani na hoja inayojadiliwa.
  • Epuka kutamka jina la unayemhoji vibaya mara kwa mara. Kma hauna uhakika wa jinsi jina lake linavyotamkwa, muulize alitamke vizuri kabla ya mjadala kuanza.
  • Kama njia ya kuonyesha heshima, ambia mtaalamu siku ama wakati ambapo kipindi mlichorekodi kitapeperushwa hewani.

Kwa mtaalamu;

  • Usizungumze na simu au kuitumia wakati wa mahojiano. Ni vizuri kuzima simu yako au kuiweka kwa namna ambayo haitafanya kele ikipiwa.
  • Epuka majibu mafupi kwani inaashiria kuwa unataja mahojiano yakamilike haraka iwezekanavyo.
  • Kumbuka kuwa ni jukumu la mtangazaji kubeba kifaa cha kurekodi na wala sio jukumu lako.
  • Epuka kudharau anayekuhoji na kumdhalilisha kama ambaye hana ufahamu wowote.
  • Usidhibiti muda. Mahojiano ni hukaribisha mazungumzo na wala sio hotuba.
  • Jibu swali moja kwa muda. Ukileta swala ambalo mwenye anakuhoji hajauliza, utakuwa unavuka mipaka.
  • Onyesha shukrani na kupendezwa na wajibu wa mtangazaji wa kuleta mazungumzo kwa msikilizaji na uonyeshe haja ya kutaka kufanya mazungumzo kuwa wazi kupitia kwa vyombo vya habari.
  • Ni kazi ya mwenye anahoji kuuliza maswali ya ziada na ya kuelezewa Zaidi kuhusu hoja inayozungumziwa. Badala ya kuonyeha kuwa hutaki aiba kama hiyo ya maswali, yapokee na uyajibu.
  • Epuka kuburi na kutaka kuonyesha kuwa wewe ndiwe unajua kila kitu.
  • Epuka kubadilisha mawazo kuhusu maswala ya kujadiliwa kwenye mahojiano na kusema nakala zako zisitumiwe.
  • Epuka kukumbusha anayekuhoji kuhusu uzoefu wako na elimu yako mara kwa mara.
  • Epuka kubadilisha maswali kama yalivyoulizwa na kuyaweka kwa njia inayokufurahisha. Kwa mfano, mwenye anayekuhoji anaweza uliza “Ni aina gani ya magugu inayoadhiri mahidi?” Epuka kugeuza swali na kuuliza “Kwa hivyo tukizungumza kuhuzu aina ingine ya mimea inayoshindana na mahidi, inayoota kabla na baada ya mahidi, ni aina gani kuu?”

4. Tumia ujuzi mzuri wa mahojiano

Kwa mwenye anahoji na mwenye anahojiwa:

  • Hakikisha kuwa maswali na majibu hayaendi nje ya mjadala.
  • Chukulia mahojiano ya redio kama mazungumzo ya ana kwa ana. Uwe na heshima na urafiki, lakini uzungumze kwa urasmi kiasi kuliko unavyozungumza na rafiki yako.
  • Muda wa hahojiano; Mara nyingi, muda unaotumika kwenye mahojiano hutegemea chanzo cha mahojiano na aina ya kipindi. Katika kipindi cha magazeti, mahojiano yaliyofanyiwa marekebisho yanafaa kuingiliana na vipengee vyengine vya kipindi. Kumbuka kuwa mahojiano ya muda wa dakika kumi na tano yanayozungumzia hoja moja yanayotolewa na mtafiti wa kilimo ama mkulima aliyebobea yanaweza kuwa na ujumbe mwingi kwa mkulima anayesikiza kufahamu na kuelewa. Badala yake, inaweza kuwa ujumbe wa kati ya dakika tatu hadi tano una manufaa Zaidi. Nchi mbali mbali hutofautiana na kile hutaja kama muda unaokunbaliwa wa mahojiano, lakini kumbuka kuwa lengo kuu ni kutoa ujumbe utakaofaa mkulima na aweze kukumbuka. Kabla ya kufanay mahojiano, fahamisha mwenye unahoji kuwa muda uliotengewa mahojiano ni kama dakika fulani na warekodi kwa muda huo ili kuepuka kufanya marekebisho mengi.
  • Kwa redio zilizo bora zaidi, wataalamu hawafai kuzungumza kwa dakika nyingi bila ya mtangazaji kuuliza maswali au kufanya mazungumzo mengine kati kati kuhusiana na hoja inayozungumziwa. Ni wajibu wa anayehoji kuingilia kati na kuzungumza kati kati ya mahojiano mara kwa mara ili kuuliza maswali, kutaka maelezo zaidi, kuongeza mtazamo wao na kuhakikisha kuwa mtaalamu hapeleki kipindi kwa kasi ili yeye pamoja na wasikilizaji waweze kuelewa.

Kwa anayehoji;

  • Uliza mtaalamu aweze kueleza maswala kwa lugha inayoeleweka zaidi bila kutumia maneno ya utaalamu yasiyoeleweka na wasikilizaji. Maneno haya magumu yasioyoeleweka sio lazima yawe ya kiufundi bali hata yale yasiyotumiwa kila siku na ni magumu kueleweka kwa msikilizaji. Kwa mfano, mtaalamu akitumia lugha ya mama lakini ahusishe maneno ya kilimo au ya afya ya lugha ya kizungu au Kiswahili, itakuwa ni vigumu kwa mkulima kuelewa. Kila mara jaribu kutumia majina bora zaidi yanayoeleweka kwa luhga ya mama au na wasikilizaji wote.
  • Patia wataalamu muda ya kutosha wa kufafanua maswala mbali mbali.
  • Epuka kulazimisha wataalamu kuegemea upande mmoja kwa maswala fulani haswa wakati kuna tofauti kali za mtazamo wa kuangazia maswala tofauti.

Kwa wataalamu;

  • Tumia lugha inayoeleweka na wasikilizaji. Kwa mfano, badala ya kusema “idadi ya waliokufa kulingana na uzoefu ni asilimia mia moja”, sema “fisi wote walikufa”. Elezea matamshi ya kiufundi ambayo hayawezi kuepukika ama yenye umuhimu wa kipekee.
  • Epuka kutoa majibu marefu yasiyo na umuhimu. Lenga kwa kutoa jawabu kulingana na muda uliopewa.
  • Usieleze mtazamo fulani kupita kiasi. Kumbuka uko hewani ili kutoa ujumbe muhimu kwa wasikilizaji.

5. Je, kunatofauti kati ya mahojiano yanayohusisha wataalamu wa kisayansi na mahojiano yanayohusisha wataalamu wa wakulima?

  • Kuna Imani potovu kuwa wataalamu wa kisayansi wanajua kila kitu kuhusu kutekeleza mahojiano murua na yenye ushawishi mkubwa. Ukweli ni kuwa baadhi ya wataalamu wamebobea ilhaliwengine hawajabobea. Wale ambao hawajabobea na wale ambao hawana ujuzi wanahitaki mwongozo wa anayefanya mahojiano iliwaweze kufanya mazungumzo yatayofaidi wasikilizaji. Kwa mfano, mtaalamu wa kisayansi anayehojiwa anaweza kukosa kuelewa kuwa mwenye anafanya mahojiano anafaa kuyadhibiti na badala yake anaweza taka kuyadhibiti mwenyewe. Wanaweza pia kukosa kuridhika wanapokatizwa mara kwa mara ili kuulizwa maswali au kutakiwa kufafanua swala fulani. Kabla ya mahojiano kuanza, wapatie muhtasari wa wanayotakiwa kufanya haswa wale wasio na uzoefu.
  • Kwa ujumla, wataalamu wa kisayansi huwa na maoni bora zaidi kuliko watafiti ilhali maoni ya wakulima husukumwa na jumbe za kila siku, uzoefu na maarifa za kale.
  • Mahojiano yanayohusisha wataalamu wa kiukulima huangazia changamoto, masaibu na hadidhi za walivyotoboa ilhali kuhoji mtaalamu huangazia jumbe za kiufundi.
    • "Tofauti kuu ni mtazamo. Mtazamo wa mkulima utaelekezwa kwa uzoefu wake ilhali mtazamo wa mtaalamu utaelekezwa kwa nadharia na uchunguzi."
  • Mtaalamu wa kisayansi hunukuu utafiti na hutoa ujumbe wa jumla kama ilivyokubaliwa na kundi la wataalamu na ujumbe huu unatarajiwa kuwa na lengo. Kwa upande wake, mtaalamu wa ukulima hutoa maarifa kutokana na uzoefu wake binafsi kwenye mandhari yake na ujumbe huu unatarajiwa kuwa na somo au mafundisho fulani.

6. Haja za kutamanika, mitazamo mbali mbali kuhusu maarifa.

  • Wakati unahoji wataalamu, tilia maanani kuwa wataalamu binafsi wanaweza kuwa na malengo ya kutimiza haja zao kando na kuanzazia kusaindia mkulima. Kwa mfano, mtaalamu anaweza kuiwa mfanyi kazi kwenye kampuni ya mbegu fulani na awe na lengo la kuinua kampuni hiyo wakati wa mahojiano. Nyakati kama hizi, ni muhimu mwenye anahoji atangaze kuwa mtaalamu anafanya kazi kwenye kampuni inayowashawishi wakulima kutumia aina fulani ya mbegu.
  • Wataalamu pia, wawe ni maafisa wa kilimo, watafiti, au wakulima wanaweza kuwa na maarifa mengi lakini huwa hawako sawa au sahihi kila wakati. Na kwa hoja moja ama nyengine, wataalamu hawa huwa hawana jawabu moja kwani hutofautiana. Ni wajibu wa anayefanya mahojiano kufahamisha wakulima na wasikizaji kuwa mbinu muhimu ambazo zitafanya kazi. Wanaofanya mahojiano husikiliza kwa niaba ya wakulima na kuhakikisha kuwa wanapeperusha noja muhimu zitakazowafaa. Hii huhusisha kuuliza maswali kwa sabau ujumbe ulio na umuhimu unaweza kuwa tofauti kutoka kwa vile mtaalamu husema ama ujumbe mtaalamu anaojaribu kupitisha kwa wasikilizaji. (Soma Viwango wastani (F.A.I.R.) vya watangazaji kwa vipindi vya ukulima, haswa kipengee cha uadilifu.)

7. Kutatua maswala mbali mbali

Mwenye anafanya mahojiano anafaa achukue hatua gani iwapo anayehojiwa anaendelea kutoa jawabu zisizo sahihi ama majibu yasiyoeleweka?

  • Uliza swali tena kwa njia tofauti.
  • Simamisha kurekodi kwa muda na uombe mtaalamu atoe jawabu zilizo sahihi. Mueleze kuwa wasikilizaji wanafaa kuelewa jibu lake kama swali lilivyouliza.
  • Iwapo kuuliza swali kwa njia nyengine hakusaidii, mwenye anafanya mahojiano anaweza uliza swali kufuatia njia zifuatazo; 1) “Hoja hiyo inavutia zaidi, lakini ninadhani ilicho cha maana zaidi kwa wasikilizaji kujua ni”…. Ama 2) “Samahani, ningetaka kueleza swala hili kwa uwazi.”
  • Iwapo mahojiano yako hewani, yamalizie haraka iwezekanavyo ili usiwaudhi wasikilizaji. Iwapo mahojiano yanarekodiwa, hakikisha umehoji mtaalamu mwengine ili kujaza nafasi ulizotaka kupata ujumbe.

Wanaofanya mahojiano wanaweza kufanya nini wakigundua kuwa mtaalamu anatoa majibu yasiyo sahihi?

  • Tafuta kujua ukweli kwa kutumia maswali mengine ama uwaulize kutoa dhibitisho la majibu yao.
  • Uliza mtaalamu iwapo jibu ni sahihi au ni maoni yao binafsi na kisha udhibitishe kwa kufanya utafiti au kutoka kwa vyanzo vya kutegemewa.
  • Subiri hadi mtaalamu akamilishe, kisha kwa upole umweleze mtazamo wako ambao umesikia kutoka kwa vyanzo vengine kisha umuombe akueleze.
  • Kwa upole uliza mtaalamu; “Unafikiriaje kuhusu mtazamo huu kuhusu swala hili kama ilivyoelezewa na”….

Mtaalamu anafaa kufanya nini wakati mtangazaji hajaweka ujumbe wa njia iliyo sawa wakati wa mahojiano?

  • Kwa njia ya urahisi, weka ujumbe kwa njia ya urahisi, na ukumbe kuwa sio mashindano, ni kaji ya kikundi.
  • Kama mahojiano yanarekodiwa, mtaalamu anafaa kueleza hali hiyo na akosoe mtangazaji.

Mtaalamu anafaa kufanya nini wakati mtangazaji ameuliza swali ambalo hana mamlaka ya kujibu kwa undani?

  • Mtaalamu anafaa kutoa ujumbe kwa ndani kadri ya uwezo wake lakini aeleze kuwa hana mamlaka ya kueleza zaidi ya hapo na aeleze ni kwa sababu gani. Aidha, mtaalamu pia anaweza kuelekeza mtangazaji kwa mwenye anaweza kujibu swali hilo kwa undani.
  • Wataalamu wanafaa kukataa kuzungumza kwa upole kuhusu maswala ambayo hawafai kuzungumza au waelekeze mtangazaji kwa walio mamlakani na wanaoweza kuwapa jawabu. Kulingana na uzito wa ujumbe, wataalamu pia wanaweza omba watangazaji wasirekodi au kuwataja kama waliotoa ujumbe fulani.

8. Kukabiliana na changamoto za kitamaduni na vikwazo vengine ili kuafikia mahojiano mazuri

Kuna zikwazo vingi ikiwemo tamaduni za kale na forodha ambazo huzuia mazungumzo yenye ukamilifu wakati wa mahojiano. Ni wajibu wa anayefanya mahojiano kujua changamoto hizi na huku akiziheshimu atafute mbinu ya kupaya ujumbe utakaofaidi wasikilizaji.

9. Wanaume kuhoji wanawake na wanawake kuhoji wanaume

(angalia pia Jinsi ya kuhudumia wakulima wa kike vizuri)

Mtangazaji wa kike na mtaalamu wa kiume:

  • Mwenye anafanya mahojiano avae nadhifu na mavazi yenye heshima.
  • Tafuta mandhari mazuri ya kufanya mahojiano pale kila mmoja atakuwa na uhuru wa kuzungumza bila kuogopa na upatie mwanamke uhuru wa kuondoka iwapo akiamua. Kwa mfano, akiona tabia zinazomtahadharisha kutoka kwa mtaalamu.
  • Hakikisha kuwa umeuliza jina na utumie njia nzuri ya kuita majina hayo. Kwa mfano, binti, bwana, bibi ya, bwaba ya, Chifu, Daktari, Profesa. Sio lazima ueleze kuwa ni wataalamu. Wapatie majina yao, wajibu wao au kazi wanayoifanya. Kwa njia hii, unaweza kuficha kuwa watu hawa ni wataalamu kwa sababu wakulima sio wataalamu.
  • Epuka vizingiti vinavyoletwa na jinsia. Kwa mfano, pale wataalamu wanatoa majina kulingana na jamii yao ama kazi za kila siku, na inakuwa vigumu kwa mhojaji wa kike kuelewa.
  • Ujiweke kwa njia ramsi na uepuke lugha ya mwili ama vitendo visivyoeleweka ma vinavyotoo ujumbe tofauti.

Mtangazaji wa kiume na mtaalamu wa kike;

  • Epuka kudhalilisha kutokana na sababu ya jinsia.
  • Ujikabidhikwa ngia rasmi na uepuke vitendo au lugha ya mwili inayoleta picha mbaya.
  • Umbali wako na ule wa mtaalamu uwe ni ule unaokubaliwa kulingana na mila na desturi.
  • Hakikisha kuwa umefanya mahijiano mchana.
  • Valia ninadhifu na mavazi yenye heshima.
  • Epuka kuiwa akina mama majina kutokana na uhusiano wao na wnaume. Kwa mfano; bibi ya, mamaya, na kadhalika ama kuwapongeza kulingana na mwonekano wao wa kimwili. Kwa mfano, wewe ni mrembo. Badala yake, tumia majina yao sahihi jinsi ungetambulisha mwanume.
  • Tambua na upongeze utendakazi wa mtaalamu na umpe heshima ambayo ungepatia mtaalamu wa kiume.

10. Jenga uhusiano bora

  • Kwa muda, uhusiano unaojengewa kwa kuweka masaa (kwa mwenye kuhoji na mtaalamu) na mwenye kuhoji akimpa mtaalamu ujumbe anaofaa kuhusu mahojiani husaindia kukuza uhusiano mwema.
  • Wanaofanya mahojiano wanafaa kukumbusha wataalamu kusikiza vipindi vya redio na waulize kupata maoni kutoka kwao kisha wajadili namna ya kushughulikia maswala ibuka.
  • Mazungumzo ya mara kwa mara yatasaindia kuondoa fikra kuwa mtaalamu huwa na maana wakati anataka kuhojiwa. Husisha wataalamu kwenye hadithi nzuri baada ya kufanikiwa.
  • Mazungumzo ya mara kwa mara pia husaindia kujenga timu n mnaweza kuanza mikutano ya kujadili vipindi au hoja muhimu.
  • Mwenye kufanya mahojiano anafaa kueleza wataalamu kuwa atawahitaji tena kwenye mahojiano ya siku za usoni na hivyo kuchukua namba za simu ili waweke mazungumzo sawa.
  • Ni vizuri kutafuta namna ya kupatia wataalamu fedha walizotumia kwenye maswala kadhaa kama nauli, kupiga simu, vyakula ila haipaswi kuonekana kama njia ya kulipa wataalamu ili kuchukua nafasi kwenye mahojiano.
  • Ili kuendelea kuelewana, mnafaa kuangazia maswala mliyozungumzia kitambo na kufanya mikutano baada ya muda.
  • Kutokana na maelewano, mtenge wakati wa kutoa maoni, kufuatilia mliyozungumza na mikakati kabambe, na mfanye mikutano ya kujadili hoja muhimu.

Ninaweza kusoma wapi tena mahojiano yanayohusisha wataalamu?

Nectary, undated. La kufanya na la kutofanya wakai unafanya mahojiano na wataalamu wa ukulima. http://nectafy.com/subject-matter-expert-interviews/

Shukrani ziendee wafuatao;

Imechangiwa na: Vijay Cuddeford, mtafsiri mkuu , kampuni kuu ya kitaifa ya Farm Radio, na Sylvie Harrison, kiongozi wa timu inayokuza redio , kampuni kuu ya kitaifa ya Farm Radio. Imechangiwa na Doug Ward, bodi ya viongozi wakuu, kampuni kuu ya kitaifa ya Farm Radio; na David Mowbray, mhojiwa mkuu, kwenye kampuni ya Farm Radio.

Vyanzo vya fahamu hizi
Wafuatao walichangia kwa njia nzuri kwa msururu wa maswali, na kusaindia kuzalisha vifaa vya maana vya kusoma kuhusu mwongozo wa kufanya mahojiano na wataalamu:

Watangazaji:
Sheila Chimphamba, Zodiak Broadcasting Station, Malawi
James Gumbwa, Malawi Broadcasting Corporation, Malawi
Izaak B. Mwacha, Radio Maria, Tanzania
Mohemedi Issa, Abood Media, Tanzania
John Mkapani, Nkhotakota Community Radio Station, Malawi
Gideon Kwame Sarkodie Osei, ADARS FM, Ghana
Koleta Makulwa, Sahara Media, Tanzania
Adongo Sarah, Mega FM, Uganda
Mubiru Ali, Radio Simba, Uganda
Oumarou Sidibe, RTB2/Bobo, Burkina Faso
Koloma Irène Sayon, Radio Kafo-Kan, Mali
Samuel T. Sawadogo, Radio Manegda, Burkina Faso

Wafanyikazi waliobobea, watafiti na wengineo:
Saulosi Kachitsa, Ministry of Transport and Public Works, Malawi
Esnarth Nyirenda, Department of Agricultural Research Services, Malawi
Fulla Yassin, Longido District Council, Tanzania
Danley Colecraft Aidoo, University of Ghana, Legon
Paschal Atengdem, University of Ghana, Legon-Accra.
Stella Aber, World Vision, Uganda
Philip Chidawati, Malawi Milk Producers Association
John Msemo, Ministry of Agriculture Livestock and Fisheries, Tanzania
Tumwesige Julius, Africa 2000 Network, Uganda
Doris Dartey, National Media Commission, Ghana
Richard Bambara, ONG LVIA, Burkina Faso
Moussa Kone, Local Service of Animal Products (SLPIA), Bougouni, Mali

Uundaji wa mwongozo huu ulipiwa jeki na kiyuo kikuu cha utafiti na ukuaji cha kitaifa cha Canada (IDRC) kupitia kikundi kikuu cha utafiti cha kuweka akiba ya chakula cha Canada. (CIFSRF).